MKUTANO MKUU WA 17 WA SHIRIKISHO LA MASISTA WAKATOLIKI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ACWECA).
Na
Pascal Mwanache
Mkutano
huo umefunguliwa Agosti 26, 2017 kwa Misa Takatifu iliyoongozwa na Rais wa
Baraza la Kipapa la Maisha ya waliowekwa wakfu Mwadhama Joao Kardinali Braz de
Aviz kutoka Vatikani.
Katika Misa Takatifu ya ufunguzi wa mkutano huo Kardinali
Joao amewaasa watawa wanaounda shirikisho hilo kutomezwa na tama ya fedha
katika utume wao na badala yake wajikite katika kutoa huduma bila kutegemeamalipo
ya hapa duniani.
Mkutano
huo wa unatarajiwa kufanyika hadi Septemba 2, 2017 katika kituo cha
mikutano cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kurasini jijini Dar es
salaam.
Umoja huo unaundwa na nchi 9 ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda,
Malawi, Zambia, Ethiopia, Sudani ya Kusini, Sudani na Eritrea. Baadhi ya wageni
waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo ni pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki
Bunda Mhashamu Renatus Nkwande, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es
salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa, na Balozi wa Papa nchini Askofu
Mkuu Marek Solczyński.
Hongereni na Bwana wetu yesu Kristu akawabariki katika utume wenu
ReplyDelete