Yesu hana mbadala wake: Askofu Nyaisonga


Na Emanuel Mayunga Sumbawanga
Padri Albert Twenya wa Jimbo Katoliki Sumbawanga na Sista Priscilla Ndegeya wa shirika la masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika wamezikwa Novemba 9 mwaka huu, huku wakiacha simanzi kubwa wa waamini wa Jimbo hilo.
Akiongoza ibada ya mazishi iliyotanguliwa na Misa Takatifu ya kuwaombea marehemu hao, Askofu Gervasi Nyaisonga wa Jimbo Katoliki Mpanda amempa  pole Askofu Damian Kyaruzi, mapadri, watawa na waamini wa Jimbo Katoliki Sumbawanga kwa msiba huo akiwataka kuhuzunika kwa imani wakipokea mapenzi ya Mungu kwa unyenyekevu.
 “Yesu hana mbadala wake na hivyo kila tunachokifanya katika imani yetu tuzidi kushikamana naye tukiwa hapa duniani kwa kufuasa mafundisho ya Mama Kanisa na kuiishi imani kila mmoja kwa nafasi yake,” amesema Askofu Nyaisonga.
Amewataka waamini kuiishi misingi ya Imani ya Kanisa Katoliki na kufuata mwongozo wa kiliturujia kadiri ya mafundisho ya Mama Kanisa kwani Yesu Kristo hana mbadala wake .
Marehemu  Padri Albert Twenya amefariki dunia Novemba  7 mwaka huu mjini Sumbawanga kutokana na maradhi ya mda mrefu akiwa na miaka 59 ya kuzaliwa na miaka  34 ya upadri.
Sista Priscilla Ndegeya amefariki dunia Novemba 6 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 89 ambapo wote kwa pamoja wamezikwa katika makaburi ya mapadri na watawa Katandala jimboni Sumbawanga.
 Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na mamia ya waamini akiwemo Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo Katoliki Sumbawanga na Abate Pambo Martin Mkorwe OSB wa Abasia ya Roho Mtakatifu Mvimwa.
Raha ya milele uwape ee Bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani, amina!


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU