Askofu Mkuu Rugambwa awa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu

Na Celestine Nyanda, Vatikani
BABA Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu Mkuu Protase Rugambwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja ya Upadri kutoka kwa Papa Yohane Paulo II alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa padri wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara.
Tarehe 18 Januari 2008 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na Juni 2012 aliteuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari.

Aidha Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Giovanni Pietro Dal Toso kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU