Jimbo Kuu Katoliki Mwanza lapata pigo


Na George Alexander, Mwanza

JIMBO Kuu Katoliki Mwanza limepatwa na simanzi baada ya kuondokewa na padri mzalendo John Buluma (90) ambaye amefariki tarehe 7 Novemba 2017 katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Jimbo Kuu Katoliki Mwanza imeeleza kuwa padri John Buluma alifariki alfajiri ya tarehe 7 katika hospitali ya rufaa Bugando alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
Aidha shughuli za kuuaga mwili wa marehemu padri John Buluma zinatarajiwa kufanyika katika Kanisa Kuu la kiaskofu la Jimbo Kuu Mwanza ( Kanisa la Epifania Bugando) siku ya Jumatatu kuanzia saa mbili kamili asubuhi ambapo mwili utawasili ukitokea katika hospitali ya rufaa ya Bugando ulipohifadhiwa na kutoa fursa kwa waamini wote kuaga.
Adhimisho la sadaka ya misa takatifu litafuata kuanzia saa nne kamili ambalo litaongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza Mhashamu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi na baadaye kumpumzisha marehemu katika makaburi ya mapadri wa Jimbo hilo yaliyopo katika seminari ndogo ya Mtakatifu Maria ya Nyegezi (Nyegezi Seminari).
Marehemu padri John Buluma ni miongoni mwa mapadri wazalendo wa Jimbo Kuu Mwanza ambao wamefanikiwa kutoa huduma za kipadri katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza na kuwapatia wakristo sakramenti mbalimbali.
Alizaliwa tarehe 29/03/1927 na kufariki tarehe 7/11/2017 na ndio alikua padri mzee kuliko wote katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU