KUELEKEA SINODI YA VIJANA: MASWALI YA VIJANA YAPO MTANDAONI HADI DESEMBA 31

Siku zilizopita kuanzia tarehe 16-17 Novemba 2017 umefanyika mkutano wa tatu wa XIV wa Baraza la kawaida la Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maaskofu akiwapo hata Baba Mtakatifu Fransisko. Shughuli hiyo ilianza na hotuba ya Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Kardinali Lorenzo Baldisseri. Katika hotuba yake alianza na salamu kwa Baba Mtakatifu  kwa kumshukuru uwepo wake, zaidi pia kwa tendo la kuhitimisha Sinodi Maalum ya Maaskofu wa  Kanda ya Amazon ambayo itafanyika mwezi Oktoba 2019.
Kardinali Baldisseri amewakaribisha washiriki wote wa Mkutano na kutoa taarifa kamili za mchakato wa Sinodi ya XIV  ya Maaskofu  kufikia leo hii, akisisitiza hasa juu ya Hati ya maandalizi na maswali ambayo yametumwa kwa wahusika wote wenye haki, pia juu ya ufunguzi wa mtandao wa moja kwa moja wa maswali kwa vijana, juu ya kuweka mikondo mingine ya kijamii, na juu ya Semina ya Kimataifa iliyokuwa inahusu hali halisi ya vijana, semina iliyofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Baada ya hotuba yake, walijadiliana kwa pamoja mantiki hiyo na kushirikishana hati ya matayarisho (dell'Instrumentum laboris) ili kuweza kupata ripoti mbalimbali ikiwa ni katika sehemu ya mchakato wa  mwisho wa kufanyia kazi. Pia  wamewasilisha  baadhi ya matokeo ya kazi iliyofanyika katika Semina ya Kimataifa na juu ya majibu ya maswali ya hali ya maandalizi ya moja kwa moja na kuonesha takwimu za mwanzo kuhusiana na maswali ya moja kwa moja katika mtandao wa kijamii. Kulingana na suala hilo la Mtandao, wametoa uamuzi wa kuacha maswali hayo katika mtandao hadi tarehe 31 Desemba 2017.
Kati ya shughuli za mipango maalumu iliyowekwa maanani pia ni juu ya Mkutano kabla ya Sinodi ya Vijana, ulioitishwa na Baba Mtakatifu kuanzia tarehe 19-24 Machi 2018. Kuhusiana na mkutano huo, wamejikita vilevile kujadili juu ya vijana watakao alikwa kushiriki Mkutano huo ambapo wamekubaliana kupanua ueleweshaji wa kushiriki kupitia mitandao ya kijamii.
Na mwisho wa Mkutano huo wawakilishi wa Baraza la Mkutano huo wamejadiliana juu ya mada ya kurudia kuangalia kwa kina sheria za Sinodi ya Maaskofu. Na kwa upande huo Monsinyo Fabio Fabene, Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu ametoa ripoti na kuonesha kazi nzima iliyofanywa na Sekretarieti Kuu ya Maaskofu ambapo wameweza kujadiliana kwa kina  na kubadilishana mawazo tofauti yenye kuleta manufaa. Mwisho wa mkutano wao wametamka rasmi tarehe ya Mkutano wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu Vijana ambao utaanza tarehe 3-28 Oktoba 2018.Wakati huo huo  Baba Mtakatifu Fransisko ametoa taarifa ya uteuzi wa Msemaji Mkuu kuwa, atakuwa Kardinali Sérgio Da Rocha na Makatibu Maalumu wawili ambao watakuwa, Padri Giacomo Costa na Padri Rossano Sala. Aidha Baba Mtakatifu Fransisko amewashukuru wanachama washiriki wa Baraza la Maaskofu na wengine kwa michango yao katika roho ya ushiriki wao kindugu walioonesha.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU