MKUTANO MKUU WA 17 WA SHIRIKISHO LA MASISTA WAKATOLIKI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ACWECA).
Na Pascal Mwanache Mkutano huo umefunguliwa Agosti 26, 2017 kwa Misa Takatifu iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Maisha ya waliowekwa wakfu Mwadhama Joao Kardinali Braz de Aviz kutoka Vatikani. Katika Misa Takatifu ya ufunguzi wa mkutano huo Kardinali Joao amewaasa watawa wanaounda shirikisho hilo kutomezwa na tama ya fedha katika utume wao na badala yake wajikite katika kutoa huduma bila kutegemeamalipo ya hapa duniani. Mkutano huo wa unatarajiwa kufanyika hadi Septemba 2, 2017 katika kituo cha mikutano cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kurasini jijini Dar es salaam. Umoja huo unaundwa na nchi 9 ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Ethiopia, Sudani ya Kusini, Sudani na Eritrea. Baadhi ya wageni waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo ni pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda Mhashamu Renatus Nkwande, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa, na Balozi wa Papa nchini Askofu Mkuu...