KUZUIA ADHABU YA KIFO KWALETA MATUMAINI DUNIANI

Wataalamu na mawaziri wa nje, wanasiasa na maaskofu wamekusanyika kwa lengo la kupiga  vita hukumu ya kifo duniani kote.


Jumapili, Papa Francis alihimiza kusitishwa kwa adhabu ya kifo na kutoa taswira ya mkutano juu ya suala hili uliofanyika Jumatatu, wenye jina la "Dunia Bila adhabu ya kifo ulioandaliwa na jumuiya ya kikristo ya Mtakatifu  Egidio.
Rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Marco Impagliazzo, alianza kwa kumshukuru Baba Mtakatifu kwa ujumbe wake wa Jumapili ili kukomesha adhabu ya kifo huku maneno hayo yakirudiwa katika video ya Papa Francis ', ambayo ilipata makofi mengi kutoka wote, ikiwa ni pamoja na mawaziri mbalimbali na mabalozi .
Wengi wa mawaziri na mabalozi walimshukuru Papa Francis kwa kutoa  uongozi katika suala hili.
Waziri wa Sheria nchini Afrika Kusini, Michael Masulha, hasa alimshukuru kwa ajili ya kusaidia kuitoa dunia katika katika matendo maovu yanayokiuka haki za binadamu na wajibu wa kujenga moyo wa huruma na ubinadamu"

Askofu mkuu wa Munich na rais wa C9 Kardinali Reinhard Marx, na kiongozi wa baraza maalum la ushauri wa Papa, alisisitiza jinsi "uwazi" na "kusisitiza" ujumbe wa Papa juu ya adhabu ya kifo. Yeye pia alikumbuka jinsi Papa alivyokuwa wazi kwa upinzani wake kwa adhabu ya kifo wakati wa Ziara ya  Kitume nchini Marekani mwezi Septemba mwaka jana.

mkuu wa Tume ya Ulaya wa Kitengo cha jinsia na Haki za Binadamu na mpito Kurugenzi ya Maendeleo ya Binadamu na Uhamiaji Jean Louis Ville, , alisema, "Umoja wa Ulaya upo mstari wa mbele katika kukomesha hukumu ya kifo duniani kote."
"Nchi zote wanachama wa jumuiya ya Ulaya wanapinga adhabu ya kifo katika hali zote," alisisitiza, "katika vita na wakati wote wa amani."

Mtandao wa ZENITH..

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU