"MAPADRI MSIKATISHWE TAMAA" ASKOFU PAULO RUZOKA
MHASHAMU Baba Askofu Mkuu Paulo Ruzoka wa Jimbo kuu Tabora amewaomba mapadri wote nchini kutoa huduma zao kwa waamini bila kuchoka wala kukata tamaa na daima wao waseme sisi ni watumishi tusio na faida tumefanya tuliyopaswa kufanya.
Askofu Ruzoka ametoa rai hiyo
wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu aliyoiadhimisha katika kanisa la kuu la
jimbo la Mtakatifu Theresia wa mtoto Yesu Tabora.
Akihubiri,Askofu amesema mapadri
hawana budi kudumu kwa uaminifu hasa juu ya ahadi walizoweka wakati walipopewa
Sakramenti ya upadrisho.
Aidha katika ibada hiyo ya Misa
Takatifu mafuta ya wagonjwa,wakatukumeni na Krisma takatifu yalibarikiwa.
“Mafuta haya tunayoyabariki ni
zana za kazi hivyo mapadre wayatumie katika kuhudumia waaamini,wapange vizuri
ratiba zao za utume ili waweze kuwatembelea wagonjwa kusikiliza matatizo yao na
kuwapa huduma ya sakramenti ili kuwapa matumaini na uhakika wa safari yao
yakumrudia Muumba wao”.
Kuhusu mwaka wa Huruma ya Mungu
ameshauri kila muumini anapaswa kutumia mwaka huu kuona na kuonja Huruma
ya Mungu kwa wanadamu na kuwa tayari kuipeleka huruma hiyo kwa wengine
akibainisha kuwa huu ni mwaka wa kupatana na kufanya toba ya kweli.
Askofu Ruzoka pia amesema
majuma sita ya kwaresima ni kipindi ambacho waamini wanapaswa kutafakari kwa
kina kuhusu ufuasi wao kwa Kristu;
Aidha amesema wanadamu
wanapaswa kuwa na moyo wa shukrani katika mafaniko yoyote kwani Mungu ndiye
mweza wa yote.
“Tuwe tayari kumuomba radhi
Mwenyezi Mungu pale tulipofanikiwa na kudhani tumeweza yote kwa uwezo wetu na
ubunifu wetu”.
Askofu Ruzoka amesema mwanadamu
anapokutana na changamoto asikate tamaa bali ajue hayuko peke yake bali yupo na
Kristu na kusanyiko kama hili ni vema liwe la kutiana moyo katika utume na kusaidiana
bila kuhubiria wengine wakati wao wakiangamia.
Askofu Ruzoka amewatia moyo
mapadri kutokata tamaa pale wanapotafsiriwa tofauti na walivyo bali watambue
kuwa hata Kristu hakupendwa na wote,ndiyo maana akateswa na kufa msalabani.
Ibada hiyo ya Misa imehudhuriwa na mapadri,watawa,waseminaristi
wakubwa(Kipalapala seminari)na waamini wa parokia ya Mtakatifu Theresia wa
Mtoto Yesu na parokia za jirani.
Na pd MamboT
Baadhi ya waamini wakishiriki Ibada ya Misa takatifu katika kanisa la kiaskofu Tabora.Na pd Mambo T.
Mhashamu Baba Askofu Mkuu Paulo Ruzoka muda mfupi kabla ya kuanza maandamano. Na pd Mambo T
Mhashamu Baba Askofu Ruzoka akichanganya manukato katika mafuta ya Krisma takatifu. Na pd.Mambo T.
Mhashamu Baba Askofu Ruzoka akipokea mafuta matakatifu.
Wanakwaya wa kwaya ya Watakatifu mashahidi wa Uganda , Tabora
safi sana jamani muweke sana mapicha haya
ReplyDeleteASANTE,karibu sana
ReplyDelete