"FUNGUENI MILANGO KWA WAKIMBIZI"PAPA AWAAMBIA VIONGOZI DUNIANI
Baba mtakatifu Papa Francis
amewataka viongozi duniani kuwaruhusu kuingia nchi mwao wakimbizi na wahamiaji
wanaokimbia kwao kutokana na vita na migogoro.
Amesema si vizuri kuwazuia kuingia
nchini watu ambao wamekimbia kwa mwendo mrefu bila kula wala kunywa,wakiwa na
hofu,maumivu na kumbukumbu za wapendwa wao waliowapoteza.
Watu hawa waweza kujiuliza Mungu
yupo wapi?inawezekanaje mateso makali hivi kuwapata watu wasiokuwa na
hatia,watoto na wanawake?amesema Papa.
Papa amesema ni faraja kuwaona
viongozi wengi na serikali zao wakifungua mioyo yao na kuwaruhusu wakimbizi na
wahamiaji kuingia nchini mwao pasipo kikwazo chochote.
Papa Francis ameyasema haya
akizungumza na karibu mahujaji 40,000 waliokuwa wakimsikiliza katika eneo la
Mtakatifu Petro.
Katika katekesi yake juu ya huruma
kwa njia ya maandiko,amelenga katika sura ya 30-31 katika kitabu cha Yeremia
ambacho pia hujulikana kama kitabu cha faraja kutokana na matumaini ambayo nabii
huyo aliyatoa kwa wafuasi wake.
Papa Francis amewaonyesha
wasikilizaji wake jinsi gani nabii Yeremia alikwenda kwa wana wa Israeli
waliokuwa uhamishoni na akawatangazia kurudi katika nchi yao.
Papa Francis ameeleza kuwa sisi pia
tuna uzoefu wa aina ya kifungo kuwa kuna wakati uzoefu wa mateso na kifo
hutufanya sisi kufikiri kwamba Mungu ametuacha.
Papa amehitimisha kwa kuomba
Mwenyezi Mungu awabariki wote wanaoishi katika hali kama hizo na kuwalinda
kutokana na maovu.
CNA/EWTN News
Vizuri Baba Mtakatifu Francis Kwan unaonyesha mfano mzuri kwa waamini wako na watu wote kwa ujumla, Mungu akuzidishie neema na baraka zake.
ReplyDelete