PAPA ALAANI SHAMBULIZI LA WOGA PAKISTANI



Papa Francis ameomboleza vifo vya watu zaidi ya 70 vilivyotokea siku ya jumapili baada ya mtu aliyejitoa mhanga kuwashambulia wakristu waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya pasaka katika eneo la wazi nchini Pakistani wengi wao wakiwa watoto na wanawake.
Akiongea wakati wa Regina Caeli juu ya sikukuu ya pasaka,Papa akionyesha kuguswa na tukio tukio la kihalifu la woga na lisilokuwa na huruma ameiomba jamii nzima kuwaombea waathirika pamoja na wapendwa wao.
“Pasaka imegubikwa na umwagaji wa damu na mauaji ya halaiki kwa watu wasio na hatia,zaidi familia za wakristu wachache,wanawake na watoto waliokusanyika kwenye eneo la wazi kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha.”Amesema
Shambulizi la kujitoa mhanga limetokea nchini Pakistani katika jiji la Lahore.Zaidi ya watu 70 wameuawa huku,zaidi ya 29 wakiwa watoto kwa mujibu wa Reuters.BBC inaripoti kuwa takaribani watu 300 wamejeruhiwa huku mamlaka zikitarajia idadi kuongezeka zaidi.
Papa amezitaka mamlaka za kiserikali kuhakikisha usalama wa umma hasa makundi madogo ya kidini huku akibainisha kuwa mashambulizi ya kikatili kawaida huacha uchungu na uharibifu mkubwa na akasisitiza kuwa uwepo wa heshima na undugu ndiyo njia ya amani ya kudumu.

VATICAN.COM

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU