TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA MWANZA
TAMASHA la Pasaka 2016 linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions jijini Dar es Salaam, linatarajia kufanyika Machi 27 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, Mkoa wa Mwanza umepata bahati hiyo baada ya wakazi wake kuomba kwa kipindi kirefu kufikiwa na tamasha hilo.“Kamati yangu huwa inasikia matakwa ya mashabiki wa muziki wa injili kwa sababu tamasha hilo ni lao ni vizuri kuwasikiliza,” alisema Msama.“Tamasha letu linawahusu wenye uhitaji maalumu ambao ni walemavu, wajane na yatima ambao misaada yao inatokana na tamasha hilo, hivyo wajipange na kujitokeza kwa wingi,” alisema Msama
Comments
Post a Comment