PAPA FRANCIS ALAANI MASHAMBULIZI BRUSSELS




Papa Francis amewaombea waathirika wote wa mashambulizi katika uwanja wa ndege nchini Ubelgiji huku akiombea amani itawale.

“wakati tukijifunza juu ya mashambulizi yaliyotokea Brussels,ambayo yameathiri watu wengi,Papa Francis ana imani na huruma ya mungu kwa watu waliopoteza maisha yao na anawaombea ndugu zao kwa vifo vya wapendwa wao”amesema Kardinali Pietro Parolin.

Katibu wa Vatican amesaini barua iliyotumwa kwa Mhashamu Askofu wa Mechelen-Brussels,Jozef de Kesel,kwa niaba ya Papa Francis.

Amesema Papa ameonyesha masikitiko makubwa kwa waliojeruhiwa,kwa familia zao na wote wanaochangia katika jitihada za kuwafariji,na amewaombea Mwenyezi Mungu awape faraja ya kudumu.

Papa Francis ameshutumu vikali vurugu zilizosababisha mateso hayo huku akimtukuza Mungu kwa tunu ya amani na kutaka Baraka zote ziwe juu ya familia na wabelgiji kwa ujumla.

Sala za Papa zimekuja baada ya takribani watu 34 kuuawa huku 170 wakijeruhiwa katika mashambulizi ya machi 22 kwenye uwanja wa ndege Brussels Zaventem na kituo cha usafiri wa treni karibu na majengo ya jumuiya ya Ulaya E.U.

Milipuko mapacha imelipuka uwanjani hapo saa 8 usiku wa manane na kusambaa katika eneo la kusafiria.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,yawezekana lilisababishwa na mtu aliyejitoa mhanga.

Vatican.com

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU