JIMBO LA MUSOMA LAADHIMISHA IBADA YA MATAWI
Baba Askofu wa Jimbo la Musoma Michael Msonganzila akisoma neno kwa waamini kabla ya maandamano ya ibada ya matawi katika kanisa kuu jimbo la musoma.
Tukio hili humaanisha Mama Kanisa anakianza Kipindi cha Juma kuu kwa Yesu kuingia Yerusalemu kwa shangwe. Hii ni shangwe ya maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii waliomtambua na kumwona Yesu kuwa ni Mwalimu maskini na mnyenyekevu, anayekuja kuwakirimia huruma ya Mungu na amani. Anapanda Punda bila ya kuwa na ulinzi wowote, anaongozwa na upendo ili kuonesha umuhimu wa majadiliano na mshikamano katika ukweli na haki na wala si kwa upanga na risasi.
Miti ya Mizeituni na mitende ni alama ya matumaini na amani, changamoto kwa waamini kuwa kweli ni wajenzi na vyombo vya amani katika medani mbali mbali za maisha. Matawi ya mitende yaliyobarikiwa ni alama ya imani kwa Mungu wa amani na maendeleo. Mti wa Mizeituni ni alama ya ibada na amani; furaha na faraja na kwamba, mafuta yake yanaupamba uso wa mwanadamu na kuondoa makunyanzi yake.
Na Veronica Modest,Musoma
Comments
Post a Comment