PICHA 16 ZA SIKUKUU YA MAPADRI WA JIMBO KUU DAR ES SALAAM LEO




Mapadri wanaohudumu katika jimbo Kuu Dar es Salaam wameadhimisha Sikukuu yao kwa Ibada ya Misa Takatifu ya Kubariki Mafuta iliyofanyika Katika Kanisa Kuu la Mt. Yosefu jimboni humo.

Adhimisho hilo limeongozwa na Mhashamu Askofu Eusebius Nzigilwa, Askofu Msaidizi wa jimbo hilo leo Jumanne, siku iliyotengwa na jimbo kuwakutanisha Mapadri wote kusherehekea sikukuu yao iliyowekwa na Yesu Kristu siku ya Alhamisi Kuu ambapo aliweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Sakramenti ya Upadri.

Pamoja na mambo mengine Mhashamu Askofu Nzigilwa amewaongoza mapadri kubariki mafuta ambayo hutumika katika maadhimisho ya Sakramenti mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mafuta ya Mpako Mtakatifu wa Wagonjwa, Mafuta matakatifu ya Krisma na Mafuta ya Wakatekumeni.

Aidha mapadri wamerudia ahadi zao za upadri, tendo ambalo limeongozwa na Mwadhama Polycap Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa jimbo hilo la Dar es Salaam.

Sikukuu ya Mapadri huadhimishwa kila Alhamisi Kuu Ulimwenguni kote ila kutokana na mahitaji Jimbo Kuu Dar es Salaam liliweka utaratibu wa kuadhimisha sikukuu hiyo siku ya jumanne lengo likiwa ni kuwawezesha Mapadri kutoa huduma katika parokia zao siku ya Alhamisi Kuu.

Sikukuu hiyo imesherehekewa na mapadri zaidi ya 300.

Adeline Berchimance

















Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU