PAPA FRANCIS RASMI INSTAGRAM:APATA WAFUASI ZAIDI YA MILIONI MOJA SIKU YA KWANZA
BABA
Mtakatifu Fransisko amezindua akaunti mpya ya picha kwenye mtandao wa
Instagram, mtandao wenye mvuto mkubwa kwa vijana wa kizazi kipya.
Baada
ya kujiunga na Instagram Machi 19, 2016 Papa tayari amepata watu milioni 1.5
wanaomfuatilia.
Akaunti
yake ina jina la @ Franciscus. Huu ni mtandao unaomwezesha Papa
Fransisko kuwashirikisha vijana wanaojikita katika mitandao ya kijamii kuona
baadhi ya picha, lengo ni kuvuka vikwazo vya lugha, ili kuwafikia watu wengi
zaidi kwa njia ya lugha ya picha inayoweza kueleweka na watu wengi zaidi.
Katika ujumbe wake
kwenye mitandao ya kijamii Papa amesema kuwa matumizi ya mtandao wa Instagram
ni hija mpya anayopenda kuitumia ili kutembea na vijana katika njia ya huruma
na upendo wa Mungu.
Baba Mtakatifu
amezindua matumizi ya mtandao huu mjini Vatikani kwa kurusha picha yake ya
kwanza inayomwonesha akisali.
Tukio hili
limehudhuriwa na kushuhudiwa na Bwana Kevin Systrom, Mwakilishi mkazi na
mwanzilishi mwenza wa mtandao wa Instagram pamoja na Monsinyo Lucio Adrian
Ruiz, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Mawasiliano mjini Vatikani.
Mwenyekiti wa
Sektretarieti ya Mawasiliano mjini Vatikani Monsinyo Dario ViganĂ² amesema kuwa kitengo cha mawasiliano ya jamii
katika Sektretarieti hii kitawajibika kuratibu akaunti ya Baba Mtakatifu katika
mtandao wa kijamii wa Instagram, hasa wakati huu wa maadhimisho ya Mwaka
Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu.
Mtandao huu utatumika
pia kuwashirikisha vijana wa kizazi kipya picha na video fupi za Baba Mtakatifu
Fransisko.
Ikumbukwe kuwa Papa
ana akaunti ya Twita yenye zaidi ya watu Milioni 27 wanaomfuatilia, wakiwemo
Rais wa Marekani Barack Obama na mwanamuziki Justin Bieber.
Chanzo: Radio
Vatikani
Comments
Post a Comment