UZINDUZI WA GROTO NA KAMUSI YA LITRUJIA YA KANISA KATOLIKI ULIVYOFANA KATIKA PICHA 15 JIMBONI DAR ES SALAAM
Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam limefanya uzinduzi wa GROTTO(kanisa
dogo) mpya ya Bikira Maria pamoja na KAMUSI YA LITRUJIA KATOLIKI, matukio
ambayo yamefanyika kwenye Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu kwa adhimisho la Misa
Takatifu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jimboni humo.
Uzinduzi huo umefanywa na Mwadhama Polycap Kardinali Pengo,
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Dar es Salaam akishirikiana na Askofu Msaidizi wa
Jimbo hilo Mhashamu Eusebius Nzigilwa pamoja na Mapadri kadhaa na waamini kwa
ujumla.
Kamusi hiyo itatumika kutoa tafsiri halisi ya maneno kama
yanavyotumika katika kanisa katoliki huku grotto ikitumika kwa ajili ya waamini
kumpelekea Mwenyezi Mungu maombi yao kupitia kwa Mama Bikira Maria.(Pichani Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizindua kamusi ya Litrujia)
Zifuatazo ni baadhi ya picha za uzinduzi huo..
Comments
Post a Comment