VYOMBO VYA HABARI VYA KANISA KATOLIKI KUWA NA SAUTI MOJA


Redio,magazeti,mitandao ya kijamii na luninga zinazomilikiwa na baraza la maaskofu katoliki Tanzania TEC,sasa vitaanza kushirikiana katika kutoa habari zenye maudhui yanayofanana ili kuifikia hadhira kubwa zaidi na kwa haraka zaidi.Sasa vyombo hivyo vitasaidiana katika kuandaa habari,vipindi,makala na kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu,utaalamu na utendaji kazi.Lengo kubwa ni kueneza injili kwa jamii kubwa zaidi,kuyafikisha kwa jamii mambo yanayofanywa na kanisa kuisaidia jamii na kuelimisha.Makubaliano haya yamefikiwa katika mkutano mkubwa wa mwaka wa mawasiliano ulioandaliwa na kurugenzi ya mawasiliano TEC na kuwashirikisha wakurugenzi wa habari majimboni,wakurugenzi wa redio za kanisa,waalikwa kutoka AMECEA pia Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano Askofu Bernadin Mfumbusa.

Comments

  1. jambo hili ni jema na la heri ambalo kwanza litaweza kusaidia hata majimbo ambayo bado havina media,pili resources haba za waandishi na pia ujumbe wa Mababa ama matukio ya kikanisa yanaweza kusambaa kwa wakati mmoja katika vyombo mbalimbali vya kanisa na kuifikia jamii kwa wakati mmoja,hongereni sana wakurugenzi kwa uamuzi huu mlioufikia mapema mwanzoni mwa mwaka huu na kikubwa tuombe utendewe kazi katika media zetu

    ReplyDelete
  2. Safi sana.Mkakati huu utavisaidia vyombo vyetu habari vya Kanisa kufanya kazi zake za upashanaji wa habari kwa ufanisi mkubwa.Hatua hii itasaidia kubadilishana uzoefu miongoni mwa watendaji. Kwa mwelekeo huu jumuiya ndogondogo nyingi za kikristo zitafikiwa na kufanya kazi ya kuipeleka injili kwa kila kiumbe kuwa rahisi zaidi.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI