BEI JUU KWARESIMA:TANGA WALIA
Na VICTOR MKELLO WA
RADIO HURUMA TANGA.
Wakazi wa mkoa wa Tanga wamelalamikia
mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali unaozidi kuongezeka katika kipindi hiki cha
kwaresima.
Akidhibitisha
hayo mwenyekiti wa soko la Ngamiani
Mohamedi Selemani amefafanua kuwa chanzo cha kupandisha bei ya
bidhaa katika soko la Ngamiani ni
kitendo cha wao kuuziwa bidhaa kwa bei
kubwa na hata kutozwa ushuru mkubwa ambapo
hupelekea kupanda kwa bei kwani
biashara kwa sasa ni ngumu na hasa katika kipindi hiki cha masika.
Hata
hivyo baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wameongelea changamoto
wanazokutana nazo katika biashara zao hasa katika kupata wateja ndani ya
soko ambapo wamesema kitendo cha serikali kuhamisha stendi ya
mabasi kwenda kange kimesababisha kukosa wateja.
Pia baadhi ya wateja akiwemo
Jeni Msumari amesema suala la ongezeko la bei hasa katika
kipindi hiki cha kwaresima kwa kusema kwamba katika kipindi cha nyuma bidhaa
zilikuwa zinauzwa kwa bei nafuu lakini wanashangaa katika kipindi hiki bei zipo juu.
Wafanyabiashara hao
wamehitimisha kwa kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
cha mfumuko wa bei kwani ushuru wanaotonzwa
ni mkubwa na hii huwalazimu wao kuamua kuongeza bei katika bidhaa
wanazouza ili waweze kurudisha
angalau faida kidogo.
Comments
Post a Comment