UNAIFAHAMU KWAYA YA PAPA?IPATE HAPA..




KWAYA ya Papa ipo Vatican na hufanya kazi zake wakati wa ibada mbalimbali na sherehe.Kwaya hii inayosemekana kuwa ilianzishwa wakati wa upapa wa Papa Gregory Mkuu,inajumuisha waimbaji nguli wanaochaguliwa kwa umakini na uangalifu mkubwa na kwaya masta.Japokuwa kuna minong’ono kuwa kwaya hii ilianzishwa wakati wa utawala wa papa Gregory,kuna ushahidi wa kihistoria kuwa kwaya hii ilishaanza shughuli zake wakati wa enzi za Upapa wa Papa Sergius 1 kwenye karne ya 8.Kwa vyovyote,kwaya hii ni moja kati ya kwaya kongwe kabisa za kidini duniani.Hata hivyo pamoja na ukongwe wake,bado ni makini katika utendaji na kutambulika.

Kwaya ya Papa siyo kama kwaya za kawaida zingine katika kanisa lolote lile,bali ni kwaya maalum na ya upekee katika baadhi ya mambo.Ipo chini ya Vatican na kazi zake huhusisha muziki,imani na ubunifu.Kwaya hujumuisha waimbaji na wapigaji wa vyombo.Kwa sasa,inajumuisha watu wa makamo 20 na wavulana 30 wa kujitolea.Watu wa makamo huwa na wajibu wa kuimba sauti za kwanza na besi wakati vijana huimba soprano na contralto.

Viongozi wa kwaya hii huwa ni wataalamu wa muziki wa injili.Tangu enzi za uanzishwaji wake,utaratibu ni kuwa kiongozi ama kwayamasta ni askofu ambaye alijua jinsi ya kuongoza imani ya kuimba nyimbo mbalimbali.Kwa sasa,kwaya inaongozwa na mtunzi wa nyimbo na ana wajibu wa kutunga nyimbo na kuongoza kwaya wakati wa kuimba.Ni kwaya inayohudumu wakati wa misa inayoongozwa na Papa,Vatican na wakati Papa anapohudhuria misa nje ya jiji la Vatican,lakini ndani ya Roma.

Licha ya kushiriki katika maonyesho mengi yao yakiwa jiji la Vatican, kwaya ya papa pia imekuwa ikushiriki katika ziara ya kimataifa katika maadhimisho mbalimbali ya Kanisa Katoliki.Kwaya ya Papa inapendwa sana na watu wengi kama ilivyo katika utendaji wake.Sauti tamu za waimbaji, kuoanisha,mienendo na maneno murua yaliyomo katika nyimbo zao,hustaajabisha kabisa.Watu wengi waliopata fursa ya kusikiliza wakati kwaya hii ikiwajibika basi huipa sifa kubwa sana.

Kwaya ya papa imepitia katika mabadiliko mengi tangu nyakati za mwanzo ilipokuwa ikianzishwa.Baadhi ya watu wamehoji utaalamu wa kimuziki wa kwaya hii na namna nyimbo zake zinavyotungwa.Wavulana hawakuruhusiwa kwenye kwaya hadi wakati wa enzi za Upapa wa Papa Pius X wakati alipoamuru wavulana wahusishwe kwenye kwaya ya Papa.Hili lilibadilisha kitu katika sauti ya kwaya ya Papa.Namna nyimbo zinavyoandaliwa pia imebadilika na sasa kwaya hii imejengwa vyema kwa masharti mepesi juu ya namna inavyojipanga kufanya shughuli zake.

Vatican.com
 


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI