MAMA TERESA KUTANGAZWA MTAKATIFU



Baba Mtakatifu Papa Francis ametangaza kuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel hayati Mama Teresa atatangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 4 mwezi Septemba mwaka huu,miezi kadhaa baada ya Papa kuthibitisha muujiza wake wa pili aliotenda.

Kutangazwa kwa Mama Teresa,ambaye alipata sifa kwa ajili ya kazi yake ya kujitolea kuwasaidia watu maskini na walio katika hali ya kupoteza maisha wanaoishi katika makazi duni huko Kolkata India,umekuwa ukitarajiwa sana na wanaomuunga mkono na itakuwa ya kuashiria Jubilee ya kanisa katika mwaka wa huruma.

Vatican ilisema katika taarifa fupi hivi karibuni kuwa Muargentina huyo alipitishwa katika kigezo cha pili cha kumpeleka kuwa mtakatifu baada ya mwanaume mmoja nchini Brazil kutibiwa uvimbe katika ubongo mwaka 2008 kufuatia maombezi ya mtawa huyo.

Alizaliwa kamaAgnes Gonxha Bojaxhiu tarehe 26 Agosti 1910 huko Skopje Macedonia,akajiunga Loreto kwa utaratibu wa watawa mwaka 1928.

Mwaka 1946 wakati akisafiri kwa njia ya treni kutoka Kolkata kwenda Darjeeling,alianzisha utaratibu wa wamisionari wa kujitolea.

Miaka minne baadaye,zikafunguliwa nyumba zaidi ya 130 duniani kote za kutoa faraja na huduma kwa ajili ya maskini,walio katika dalili za kifo,wagonjwa na maskini wa kutupa.

The Guardian.com
 

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI