KIFO CHA MAMA ANGELICA;BENEDICT WA 16 ATOA NENO
Kifo chake kimesababisha kumbukumbu kubwa maeneo mbalimbali duniani.
Huko Roma,mkuu wa sekretarieti ya mawasiliano Monsignor Dario Vigano ameahidi kufanya maombi maalum kwa kifo cha mama Angelica.Mapadri,walei na viongozi wa kidini Roma wanamwombea kwa ajili ya kifo chake.
Askofu Mkuu Joseph Kurtz wa Louisville na rais wa baraza la maaskofu Marekani amesema mama Angelica alikuwa mwanamke wa aina yake,muumini,mcha Mungu na moja kati ya waanzilishi wa vyombo vya habari.
Kristina Arriaga , mkurugenzi mtendaji wa Mfuko Becket wa Uhuru wa Kidini , amesema sista atakumbukwa kama " mfano wa kuigwa wa ujasiri na imani ."
CNA
Comments
Post a Comment