PAPA FRANCIS AOSHA MIGUU WAISLAMU,WAKRISTU,WABUDHA..

Baba Mtakatifu Francis ameosha miguu ya wahamiaji 11 wakiwemo waislamu watatu,wakristu wanne,waorthodox,wahindu na volunteer mmoja mjini Rome katika tukio la unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa msimu wa Pasaka.
Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa pasaka.
Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana na kuwepo kwa wahamiaji hasa kufuatia mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi karibuni huko Brussels Ubelgiji.
Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu cha kumwaga damu ya binadamu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa waliyosababisha.
Aidha Baba Mtakatifu amewashauri watu wa dini tofauti duniani kuishi kwa amani.
''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu alisema Papa Francis.

BBC,ZENITH ORG

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU