SHERIA MPYA YA NDOA: PAPA AWATAKA MAKUHANI KUWA KARIBU ZAIDI NA WANANDOA
Ninayo furaha ya kukutana nanyi wakati wa kuhitimisha kwenu mafunzo kwa wahudumu wa Kanisa na walei, mkutano ulioandaliwa na Mahakama Kuu ya Vatican, ukiwa na kauli mbiu Mchakato mpya wa ndoa na hatua zake kwa ngazi zake za juu ni Mafunzo yaliyofanyika Roma, kama pia mafunzo yanayofanyika katika majimbo mengine. Mafunzo haya ni ya kupewa sifa na kutiwa moyo ili yaweze kutoa mchango na fursa ya utambuzi katika kubadilishana uzoefu kwa ngazi mbalimbali za Kanisa na umuhimu wa hatua za michakato ya sheria. Ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Fransisko Jumamosi 25 Novemba 2017 alipokutana na washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mahakama kuu ya Vatican. Baba Mtakatifu katika hotuba yake anasema, ni muhimu kutazama kwa makini Hati mbili za hivi karibuni zinazohusu “Yesu Kristo Hakimu mwenye huruma” ijulikanayo kama “Mitis Iudex Dominus Iesus” na ile ya “Huruma katika hukumu” maana yake, “Mitis et Misericors Iesus” iliyochapishwa tarehe...