Posts
Showing posts from March, 2016
MAADHIMISHO MAZITO NA MATAKATIFU SANA YA PASAKA
- Get link
- X
- Other Apps
Kanisa linaadhimisha Sherehe ya Pasaka kwa namna ya pekee sana katika Liturujia yake, wala hakuna sherehe nyingine yenye maadhimisho mazito kama hayo tunayoadhimisha Pasaka. Uzito wa Maadhimisho ya Pasaka unatokana na matendo makubwa yanayoadhimishwa katika sherehe hiyo yaani mateso , kifo na hatimaye ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristu. Pamoja na kuadhimisha matendo hayo yaliyo kilele cha ukombozi,kanisa huadhimisha matendo makubwa ambayo Yesu aliyafanya kabla ya kuanza kwake mateso,ambayo ni kula Karamu ya mwisho na mitume wake na katika nafasi hiyo aliweka Sakramenti za Ekaristi,Daraja takatifu na amri ya mapendo.Kanisa huadhimisha matendo hayo makuu ya Pasaka katika Siku tatu kuu za Pasaka. Licha ya kujiandaa kwa mfungo wa siku arobaini Juma moja kabla ya kuadhimisha ufufuko wa Bwana, kanisa linaanza rasmi kuadhimisha mateso ya Bwana katika Dominika ya Matawi ya Mateso ya Bwana .Kutokana na uzito wa kuadhimisha mateso na kifo cha Bwana, kanisa limetoa jina maalum kwa juma...
KIFO CHA MAMA ANGELICA;BENEDICT WA 16 ATOA NENO
- Get link
- X
- Other Apps
Benedict wa 16 ametoa ujumbe juu ya kifo cha mama Angelica kilichotokea katika sikukuu ya pasaka akisema “ NI ZAWADI ” Askofu Mkuu Georg Ganswein ambaye ni katibu wa Benedict wa 16 ameuambia mtandao wa CNA juu ya ujumbe wa Papa mstaafu Benedict wa 16. Mama Angelica ambaye ni mzaliwa wa Ohio,alikuwa mwanzilishi wa mtandao wa kikatoliki ulimwenguni wa EWTN huko nchini Marekani mwaka 1981.Baadaye ukaja kuwa mtandao mkubwa wa dini duniani.Amefariki dunia machi 27 katika sikukuu ya pasaka akiwa na miaka 92. Kifo chake kimesababisha kumbukumbu kubwa maeneo mbalimbali duniani. Huko Roma,mkuu wa sekretarieti ya mawasiliano Monsignor Dario Vigano ameahidi kufanya maombi maalum kwa kifo cha mama Angelica.Mapadri,walei na viongozi wa kidini Roma wanamwombea kwa ajili ya kifo chake. Askofu Mkuu Joseph Kurtz wa Louisville na rais wa baraza la maaskofu Marekani amesema mama Angelica alikuwa mwanamke wa aina yake,muumini,mcha Mungu na moja kati ya waanzilishi wa vyombo vya habar...
PAPA ALAANI SHAMBULIZI LA WOGA PAKISTANI
- Get link
- X
- Other Apps
Papa Francis ameomboleza vifo vya watu zaidi ya 70 vilivyotokea siku ya jumapili baada ya mtu aliyejitoa mhanga kuwashambulia wakristu waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya pasaka katika eneo la wazi nchini Pakistani wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Akiongea wakati wa Regina Caeli juu ya sikukuu ya pasaka,Papa akionyesha kuguswa na tukio tukio la kihalifu la woga na lisilokuwa na huruma ameiomba jamii nzima kuwaombea waathirika pamoja na wapendwa wao. “Pasaka imegubikwa na umwagaji wa damu na mauaji ya halaiki kwa watu wasio na hatia,zaidi familia za wakristu wachache,wanawake na watoto waliokusanyika kwenye eneo la wazi kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha.”Amesema Shambulizi la kujitoa mhanga limetokea nchini Pakistani katika jiji la Lahore.Zaidi ya watu 70 wameuawa huku,zaidi ya 29 wakiwa watoto kwa mujibu wa Reuters.BBC inaripoti kuwa takaribani watu 300 wamejeruhiwa huku mamlaka zikitarajia idadi kuongezeka zaidi. Papa amezitaka mamlaka za kiserikali kuhak...