MAANDALIZI YA KONGAMANO LA EKARISTI YAMEKAMILIKA
ASKOFU MSAIDIZI wa Jimbo la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini akiongea na waandishi wa habari mapema leo juu ya kongamano la tatu la kitaifa la Ekaristi Takatifu jiji Mwanza.
yupo katikati Pichani.kushoto ni Padiri - Titus Ngapemba - Katibu wa habari jimbo kuu la Mwanza na kulia ni Bernard James – Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano TEC.
Sehemu ya wanahabari
yupo katikati Pichani.kushoto ni Padiri - Titus Ngapemba - Katibu wa habari jimbo kuu la Mwanza na kulia ni Bernard James – Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano TEC.
Sehemu ya wanahabari
Usiache kufuatilia maelekezo ya kiongozi
huyo kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuanzia sasa lakini kikubwa ni kwamba.
Baraza la maaskofu
Tanzania Tec limesema vita dhidi ya mauji,manynyaso na ukiukwaji wa haki za
binadamu vinayoshuudiwa nchini si tu vinahitaji ushiriki wa kila mtu bali maombi
ya dhati ili kulinuru taifa na hali hiyo.
Akizungumza mapema leo na waandishi wa habari mkoani Mwanza
kwa niaba ya baraza la maaskofu Tanzania askofu msaidizi wa jimbo katoriki la
Bukoba Methodius Kilaini amesema kanisa
katoriki linafadhaishwa na matukio hayo ya kiharifu yanayopoteza uhai wa watu
wasio na hatia.
Amesema “Ni vitendo
vyenye kustahili kukemewa na kila mpenda amani
lakini anasema hiyo haitoshi tu bado yanahitajika maombi ya dhati kila
mtu kwa imani yake ili kuliongoza taifa katika misingi sahii”.
Anasema kanisa katoriki limeifanya amani na mwelekeo wa
taifa la Tanzania kuwa miongoni mwa masuala yatakayopewa kipaumbele katika
ibaada rasmi itakayofanyika wakati wa kongamano la ekaristi takatifu june 11
mwaka huu jijini Mwanza.
Ni kongamano litakalo dumu kwa takribani muda wa siku nne likihusisha kuyajadili
na kuyaombea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa.
Katika taratibu
za kikanisa, tukio la ekaristi ndilo tukio kubwa kuliko yote katika misingi ya
kanisa katoriki, awamu hii likifanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mara ya tatu
kufanyika nchini Tanzania, ambapo pamoja
na mambo mengine waumini,maaskofu,mapadri na watawa watakusanyika kuomba
matumaini mapya kwa jamii na familia
nyingi zilizokata tama.
Akizungumzia
suala la utendaji wa Rais Magufuli askofu Kilaini amesema ni mapema sana
kumnyooshea mkono kiongozi huyo kwani miezi sita haitoshi kupima uwezo wa mtu
aliyepewa kuliongoza taifa kwa miaka mitano.
Mwisho.
Comments
Post a Comment