ZIARA ARMENIA:PAPA FRANCISKO KABAINISHA HAYA..
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kupokewa mjini Yerevan Armenia Ijumaa hii , majira ya saa tisa na nusu saa za armenia, alikwenda kutolea sala zake katika Kanisa Kuu la Kitume la Armenia la Mtakatifu Etchmiadzin , mwenyeji wake akiwa ni Mtakatifu Karekin II, Patriaki Katolikos wa Armenia yote wakiwepo pia kikundi cha waalikwa wapatao 100.
Katika hotuba yake mahali hapo Papa Francisko , alikiri kuguswa na mahali hapo alipopataja kuwa ni hazina ya Utakatifu na ushuhuda wa historia ya watu wa Armenia na kituo chenye kutoa miali ya kiroho . Kwake Papa anaichukulia ziara hii kuwa ni zawadi ya thamani kutoka kwa Mungu, iliyomwezesha kuyaendea madhabahu hayo Matakatifu yanayotoa mwanga wa kiroho kwa watu wa Armenia.
Baba Mtaktifu Francisko aliendelea kumshukuru Bwana kwa mwanga huu unaolisha imani ya nchi hii, na kuipa Armenia utambulisho wa kipekee, katika kushuhudia Ushindi wa Kristo pia katika mataifa mengine . Kristo aliye utukufu na mwanga wa nchi ya Armenia. Kristo nuru inayowamulikia, kuwainua , kufuatana nao, na kuwadumisha na hasa katika nyakati za majaribu. Kwa ajili iyo Papa alisema kwa unyenyekevu mkuu, anainama mbele ya huruma ya Bwana , aliyependa Armenia liwe taifa la kwanza la Kikristo tangu mwaka 301, kutangaza kuwa Nchi ya Kikristo, licha kwamba kulikuwa bado kuna madhulumu makali ya himaya yote ya Kirumi.
Papa ameizungumzia historia ya Ukristo nchini Armenia , akilitaja ni kama vazi lake lenye kutoa utambulisho wake muhimu, na hivyo inakuwa ni zawadi kubwa muhimu iliyokubaliwa kwa furaha na kuhifadhiwa kwa jitihada kubwa na nguvu zote , hata kwa gharama ya maisha ya Waarmenia.
Aidha Baba Mtakatifu ameshukuru Mungu kwa safari inayowezesha kanisa Katoliki na Kanisa la Kitume la Armenia kutembea pamoja katika uweli na mazunguzano ya kidugu , ksms ilivyo sasa wanashiriki pamoja kikamilifu katika Ibada ya Misa Takatifu. AliombabBaraka za Mungu akisema” Bwana awabariki kwa ushuhuda huu unaoangazia imani. Ni mfano wa ufanisi wa kuigwa na wote waliopokea ubatizo katika taifa hili kwa zaidi ya karne kumi na saba, pamoja na ufasaha wa utakatifu wa ishara za waliuwa kama mashahidi, wa dini ambao daima wamekuwa wakiongozana na historia ya watu wa Armenia.
Papa alimemwomba Roho Mtakatifu aendeleee kutoa msaada wake katika kudumisha umoja alioomba Bwana , ili wafuasi wake wawe na umoja ili dunia ipate kusadiki.
Papa ametaja jinsi dunia ya nayakati hizi ilivyomezwa na migawanyiko na mizozoz na pia kila aina ya umaskini wa kiroho na kihali , ukiwemo unyonyaji wa binadamu na hsa watoto na watu wazee. Amenyesha tumaini lake kwamba Wakristo kwa pamoja wataweza toa uhuhuda wao dhdi ya hayo kw anjia ya ushirikiano na udugu unaoweza kuiinua kila dhamiri ya mtu kupitia uwezo na ukweli wa Kristo Mfufuka.
Papa Alikamilisha hotuba yake kwa kuomba baraka za Mwenyezi Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na maombezi ya Maria Mtakatifu sana, Mtakatifu Gregori Mwangavu, nguzo ya mwanga kwa ajili ya Kanisa Takatifu la Armenia na Mtakatifu Gregory wa Narek, Mwalimu wa Kanisa kwa taifa zima la Armenia, ili liendelee kudumu katika kumshuhudia Kristo.
Comments
Post a Comment