Jumuiya ya Kimataifa ishikamane ili kupambana na changamoto mamboleo
Tunawezaje sasa kujenga maisha ya siku za usoni yenye kukirimiana na kushirikishana, iwapo dunia inaonekana kushamiri kwenye mipasuko na kinzani? Tunawezaje leo kulisha wanyonge na kusimamia wokovu kutoka kwenye baa la njaa, iwapo dunia inayoonekana leo kuwa kama kijiji kufuatia maendeleo ya utandawazi, ndiyo dunia hiyo hiyo inayojidhihirisha kwa mmong’onyoko wa maadili na tunu njema. Maswali haya yanarushwa na Dr. Olav Fykse Tveit, Katibu mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, katika kuhitimisha Jukwaa la Uchumi na Biashara duniani, Wolrd Economic Forum , lililofanyika hivi karibuni huko Davos, nchini Uswiss, tarehe 22 – 26 Januari 2018. Maswali haya yamekuwa kama mwiba kwenye miili na mioyo ya washiriki wengi katika Jukwaa hilo, ambalo lilihudhuriwa na viongozi na watendaji wengi wa serikali, siasa, fedha na uchumi, jamii, usalama na dini kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni. Jukwaa hilo limefanyika wakati muafaka, anasema Dr. Olav Fykse Tveit, wakati ambapo dunia inaoneka...