Posts

Showing posts from June, 2016

MAGAZETI LEO ALHAMISI JUNE 30

Image

KUMBUKUMBU YA UPADRISHO WA MAPADRE 6 JIMBO KUU MWANZA..LEO

Image
PICHA ZOTE NA GEORGE ALEXANDER..

UPADRISHO JIMBO KUU MWANZA MUDA HUU...

Image
UPADRISHO:Baba Stephen Bikolwamungu,Vetrine Sumila,Daniel Kadogosa,John Kasembo,Kevin Mkama,Stephano Kilabyo,wamepadrishwa leo katika parokia ya Kawekamo,Jimbo kuu Mwanza Picha zote na George Alexander,Mwanza

SHEREHE YA WATAKATIFU PETRO NA PAULO NA FUNZO KWA JAMII

Image
Maadhimisho ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo iwe ni fursa ya kuendelea kuimarisha uhusiano, umoja wa Wakristo pamoja kuwanufaisha binadamu wote. Ni nafasi ya kukumbuka ushuhuda wa pamoja uliofanywa na viongozi wa Kanisa la Kiorthodox na Kanisa Katoliki kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji huko Lesvos, nchini Ugiriki. Wote hawa wanahitaji kuhakikishiwa usalama wa maisha yao, amani na utulivu na kwamba, wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji ni changamoto kubwa kuwahi kutokea baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Kuna watu wengi wanaoendelea kuteseka na kunyanyasika, wengi wao wakiwa ni wale wanaotoka huko Mashariki ya Kati. Ni wajibu wa Makanisa kusikiliza kilio cha wale wanaoteseka na kupondeka moyo; wahanga wa vitendo vya misimamo mikali ya kidini, ubaguzi, dhuluma, ukosefu wa haki jamii, umaskini na baa la njaa duniani. Wote hawa wanapaswa kuoneshwa mwanga wa matumaini katika maisha yao kwa kutambua kwamba, hawa ni binadamu na maisha yao ni matakatifu. Hii n...

Fumbo la Msalaba ni chemchemi ya neema na baraka!

Image
Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI amewashukuru viongozi wa Kanisa waliowezesha kufanikisha kumbu kumbu ya miaka 65 yangu walipopewa Daraja Takatifu la Upadre. Anamshukuru kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu Francisko anayeendelea kumshangaza katika maisha yake kutokana na wema na uzuri unaopamba moyo wake kuliko hata bustani za Vatican na kwamba, anajisikia kuwa analindwa na kutunzwa vyema. Anamtakia heri na baraka tele katika hija hii ya maisha ya huruma ya Mungu kwa kuwaonesha watu Yesu anayewapeleka kwa Mungu. Papa mstaafu Benedikto XVI amewashukuru viongozi wote wa Kanisa waliotoa hotuba ambazo kweli zimegusa wito na maisha yake na jinsi ambavyo alijitahidi kutekeleza dhamana na wito huo wa kipadre. Amewashukuru kwa upendo na urafiki ambao wamemwonjesha katika maisha. Kwa namna ya pekee kabisa amemshukuru Kardinali Gerhard Muller kwa kuzindua kazi zake kuhusu wito na maisha ya kipadre, ili kuwasaidia ndugu zake katika Daraja takatifu anapoendelea na maisha yak...

Miaka 65 ya Upadre imesimikwa katika huduma ya imani na mapendo!

Image
Mama Kanisa anamwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa zawadi na wito wa Daraja Takatifu la Upadre alilomkirimia Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, miaka 65 iliyopita. Huu ni wito kama ule ambao Yesu alimwangalia Simoni kwa jicho la upendo na kumuuliza ikiwa kama alikuwa anampenda zaidi kuliko wengine wote, kiasi cha kumkabidhi dhamana ya kuchunga na kulinda kundi la Kristo. Wito huu ndio umekuwa ni kielelezo cha huduma ya Kipadre na taalimungu ya kweli ya kumtafuta Kristo, ushuhuda ambao umeoneshwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto katika maisha na utume wake, ili aweze kufahamika na kupendwa zaidi, upendo ambao unaijaza nyoyo ya waamini amani na utulivu hata wakati wa shida na magumu ya maisha, kama hata ilivyotokea katika maisha ya Mtakatifu Petro. Changamoto ni kuangalia mbele kwa matumaini na furaha pasi na kujutia yale yaliyopita. Hii ni sehemu ya hotuba iliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 6...

MAGAZETINI LEO JUMATANO JUNE 29

Image