Wingi wa maji si hoja katika ubatizo
Katibu
Mkuu wa Jimbo Katoliki Morogoro Padri Luitfrid Makseyo amesema, Sakramenti ya
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni sakramenti ambayo inamuondolea mtu dhambi ya asili
na kumtayarisha kupokea sakramenti nyingine za Kanisa ili kupata uzima wa
milele.
“Kama
tukifikiri wingi wa maji ndiyo unaomtakasa mwanadamu maana yake tunaiweka akili
yetu kuamini kwamba dhambi ya mwanadamu imekaa kwenye ngozi yake, na ndiyo
maana wengine wanazamishwa kwenye maji ili wingi wa maji uweze kuwatakasa na
kuwasafisha, dhambi si kama matope.”
Padri
Makseyo amesema hayo hivi karibuni katika adhimisho la Misa Takatifu sherehe ya
Ubatizo wa Bwana katika Kanisa la Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili iliyopo
Jimboni humo.
Padri
Makseyo amesema kuwa, Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni tofauti kabisa na ubatizo wa
Yohane ambao ni ubatizo wa toba unaomwezesha mtu kutambua kuwa yeye ni
mdhambi na anaweka makusudio ya kutokutenda dhambi tena.
Aidha
amesema kuwa ubatizo huo wa Yohane wako watu wengi katika madhehebu yao bado
wanaufuata mpaka leo hii, wanapohitaji kubatiza watu lazima
wabatizwa wapelekwe mtoni kwenye mabwawa au kuwapeleka katika visima vyenye
maji mengi, akisema kuwa wingi wa maji si kigezo cha kumuondolea mtu dhambi.
Ameeleza
kuwa, wingi wa maji siyo hoja ya msingi katika ubatizo, isipokuwa nguvu ya Roho
Mtakatifu ndiyo kigezo katika utaratibu wa ubatizo wenyewe.
Nguvu
ya Roho Mtakatifu ndiyo inayoshuka na kumuondolea mtu dhambi zake kupitia
sala inayotolewa na mbatizaji, ambapo maji ni ishara wazi inayoonekana katika
tukio la ubatizo ili kuleta utakaso wa mbatizwa.
Hata
hivyo padri Makseyo amewaasa waamini kuondokana na dhana ya kudhani kwamba
wingi wa maji ndiyo unaomtakasa mwanadamu, maana yake inamfanya mwanadamu aweze
kuamini kwamba dhambi zake ziko kwenye ngozi au mwili wake, kumbe dhambi si kama
matope na wingi wa maji si hoja katika ubatizo
Amewaasa
waamini kutambua dhana nzima ya maana ya ubatizo kwamba Kanisa linasisitiza
kuwa wazazi wanapaswa kuwabatiza watoto wao mapema zaidi mara baada ya kuzaliwa
ili kumuondolea mtoto dhambi ya asili, hivyo wasimezwe na mafundisho ya mkopo
yatolewayo na makanisa mengine kwamba mwanadamu anapaswa kubatizwa akiwa katika
umri mkubwa
“Ubatizo
ni wakati wowote mtu anapoomba kupata ubatizo hakuna kipimo cha wakati, kama
sisi wakatoliki tukiwaacha watoto wanakaa muda mrefu bila kubatizwa ni makosa.
Kanisa halijafundisha hivyo, Kanisa linamtaka mtoto hata mara baada ya siku ya
tatu za kuzaliwa anaweza kubatizwa, ni vyema zaidi mtoto aondolewe dhambi
ya asili mapema” amesema.
Comments
Post a Comment