Askofu Minde ahimiza nidhamu na utii kwa watawa
Na Patrick Mabula, Kahama.
Askofu wa Jimbo
Katoliki Kahama Mhashamu Ludovick Minde amewaasa watawa kuwa na nidhamu kwa Kanisa katika utume wao.
Amesema hayo katika
Ibada ya Misa Takatifu ya kusherehekea Jubilei ya miaka 25 ya kumshukuru Mungu
kwa Masista wanne wa shirika la Mtakatifu Fransisko wa Asizi na mmoja aliyekuwa akiweka nadhiri za daima iliyofanyika katika
Parokia ya Mtakatifu Luka Mwinjili jimboni humo.
“Hakuna upadri au
utawa bila Kanisa, hilo lazima lifahamike wazi. Lazima wote tuwe na utii na
nidhamu kwa sababu miito yote ni kwa ajili ya Kanisa katika kumtumikia Mungu na si vinginevyo.
Katika maisha ya wito kuna muunganiko
kati ya Kanisa na Yesu Kristo. Hivyo watawa waone muunganiko huo katika utume
wao ili ung’are
kwa matendo na mwenendo wao,” amesema.
Askofu Minde amewasihi watawa kuishi
maisha ya neema ili uwavute wengine kuingia kuwa wito huo wakijiunganisha na Kanisa na
Kristo.
Aidha watawa wakumbuke kuwa wana wajibu wa
kujikita katika
utume wao kwa Kanisa na kwa jimbo bila makandokando.
Amewaasa waamini
kuwaombea Maaskofu, Mapadri na Watawa ili waweze kuwa watumishi wema na
kuwavuta watu kuingia katika miito ya upadri na utawa Kanisa lipate watumishi.
Kwa upande wake Msimamizi
wa Watawa wa Jimbo Katoliki Kahama Padri David Mwangu amesema kuwa, watawa ni
zawadi ya Mungu kwa Kanisa , wajifunze kusikia sauti ya Mungu na kujitoa kwa
kumtumikia katika Kanisa lake mahalia.
Watawa waliyo
sherehekea miaka 25 ya utawa ni Mama Mkuu wa Shirika hilo Frasisko wa Asizi,
Sista Bernadetta Musibimana, Sista Liberatha Mukantwari, Sista Christina Kasana
, Sista Esther Nyawile na aliyeweka nadhiri za daima ni Sista Bertha Manyanda.
Comments
Post a Comment