Mtawa afariki Kahama
Jimbo Katoliki Kahama
limepatwa na simazi baada ya kufiwa na
Sista Elizabert wa shirika la
Wamisionari wa Masista Wabenediktine aliyefariki hivi karibuni baada gari yake aina ya Land Cruser kuanguka katika
eneo la Kanegere alipokuwa katika kazi
zake za kitume .
|
Akizungumza katika Misa
Takatifu ya kumuombea Marehemu Sista Elizebert, Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama
Mhashamu Ludovick Minde amesema kuwa, kifo hicho wamekipokea kwa mshtuko,
simanzi na majonzi .
“Sista Elizabert
alimpenda Yesu , alimpenda Mungu na hakuacha njia ya utume wake katika Kanisa.
Kifo chake kimenisikitisha kwasababu
amefariki ghafla lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya sista huyu aliyekuwa anajitoa katika utume wake kwa kumtumikia Mungu na waumini wote bila
ubaguzi na alilipenda Kanisa,” Amesema
Askofu Minde katika Misa Takatifu ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la
Ekaristi Takatifu Parokia ya Kabuhima.
Comments
Post a Comment