Kazi ya UWAKA ni kuimarisha familia, Kanisa-Askofu Chengula
ASKOFU Evarist
Chengula(IMC) wa Jimbo Katoliki Mbeya
amewaalika Umoja wa Wanaume Kanisa Katoliki(UWAKA) kuwa watu wa msamaha
kwa wenzi wao na chachu ya miito kwa ajili ya Kanisa .
Askofu Chengula
ametoa wito huo wakati wa
Ibada ya Misa Takatifu ya Siku kuu ya
Mt.Yoseph Mfanyakazi iliyoambana na
uzinduzi wa Umoja wa wanaume katrika Parokia ya Ruanda.
Amesisitiza kuwa, vyama vya kitume ndiyo
mishipa ya damu ya ukombozi katika
Parokia yeyote .
“Ninawaomba
sana mtumie nafasi hii ya kusaidiana ili
kudumusha umoja huu ambao ninaamini utaleta mageuzi na mabadiliko kuanzia mtu
binafsi, familia zenu, jumuiya ndogondogo na parokia.
Uhai
wa chama chenu utategemea kwanza juhudi zenu nyie wanaume mkishirikiana na
akina mama.
Muwe
chachu ya miito katika familia zenu, jumuiya na parokia.
Pia
muimarishe familia zenu kwa fadhila ya msamaha. Muwasamehe wake zenu, watoto na
kuwa wapatanishi katika Kanisa,” amesisitiza .
Amesema kuwa endapo Uwaka itafanya kazi ipasavyo itasaidia kwa
asilimia kubwa kuondoa ama kumaliza kabisa changamoto za wazazi kuwafukuza
watoto wanaokimbilia mitaani.
Asante sana. Tunatumia Elimu hii katika jumuiya kanda
ReplyDelete