UJUMBE WA VATIKANI KUHUDHURIA JUBILEI YA UPADRI DODOMA

  Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Askofu Mkuu Protase Rugambwa, ambaye ni Katibu Mwambata na Rais wa Mashirika ya Kitume ya Kipapa.(Maktaba)

n Na Pascal Mwanache, DSM
KUELEKEA kilele cha Jubilei ya Miaka ya upadri Tanzania, imethibitika kuwa katika sherehe hiyo Mkuu wa Idara ya Uinjilishaji Vatikani Kardinali Fernando Filoni atawakilishwa na Katibu Mwambata na Rais wa Mashirika ya Kitume ya Kipapa, Askofu Mkuu Protas Rugambwa.
Hayo yamebainishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, katika mwaliko wake kwa maaskofu wa kuhudhuria kilele cha jubilei hiyo itakayofanyika Agosti 15 jimboni Dodoma.
Askofu Kinyaiya pia ameeleza kuwa katika sherehe hiyo Balozi mpya wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski anatarajiwa kujitambulisha rasmi kwa waamini nchini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa ajili ya maadhimisho hayo, Misa Takatifu ya uzinduzi wa jubilei hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 14 na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhashamu Joseph Mlola, na baada ya misa zitafuata semina mbili zitakazowezeshwa na Askofu Desderius Rwoma wa Jimbo Katoliki Bukoba na Padri Titus Amigu wa Jimbo Katoliki Lindi.
Misa Takatifu ya kilele cha jubilei inatarajiwa kuongozwa na Askofu Mkuu Protas Rugambwa ambapo pia baada ya misa atabariki jiwe la msingi la kikanisa katika makao mapya ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) jimboni Dodoma.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU