UN: Watoto takribani 12,000 wameuawa kwa vita 2018
TAkwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba,
katika kipindi cha Mwaka 2018 watoto zaidi ya 12, 000 wameuawa na wengine
kupata ulemavu na majeraha ya kutisha kutokana na vita, kinzani na misigano ya
kijamii na kisiasa sehemu mbali mbali za dunia.
Lakini maeneo
yaliyoathirika zaidi ni Afghanstan, Palestina, Siria na Yemen.
Baba Mtakatifu
Fransisko, hivi karibuni aliyaelekeza mawazo yake nchini Yemen ambako watu
wanateseka kutokana na vita, njaa, magonjwa na umaskini wa hali na kipato.
Kilio cha watoto na
wazazi wao, kinamfikia Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo. Baba
Mtakatifu ametumia fursa hiyo kutoa mwaliko kwa viongozi wanaohusika pamoja na
Jumuiya ya Kimataifa katika ujumla wake ili kutekeleza mikataba ya kimataifa
iliyotiwa sahihi pamoja na kuhakikisha kwamba, wananchi wanagawiwa chakula
pamoja na kuendelea kujikita katika kutafuta na kudumisha ustawi, maendeleo na
mafao ya wengi.
Baba Mtakatifu
wamewaombea watoto ambao wanateseka na kufa kwa baa la njaa na kiu ya kutisha;
watoto wanaofariki mikononi mwa mama zao pasi na huduma bora ya afya; hawa ni
watoto wanaonyemelewa na kifo wakati wowote ule.
Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na
watu wote wenye mapenzi mema, kuwakumbuka katika sala watoto hao.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba,
katika kipindi cha Mwaka 2018 watoto zaidi ya 12, 000 wameuawa na wengine
kupata ulemavu na majeraha ya kutisha kutokana na vita, kinzani na misigano ya
kijamii na kisiasa sehemu mbali mbali za dunia.
Lakini maeneo
yaliyoathirika zaidi ni Afghanstan, Palestina, Siria na Yemen. Takwimu hizi
zimetolewa hivi karibuni wakati Umoja wa Mataifa ulipokuwa unajadili kuhusu
usalama wa watoto wadogo katika maeneo ya vita sehemu mbali mbali za dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Bwana Antònio Guterres ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na
vifo vya watoto wadogo katika maeneo ya vita.
Umoja wa Mataifa
unasikitika kusema kwamba, kuna idadi kubwa ya watoto wadogo wanaopelekwa
mstari wa mbele kama chambo wakati wa vita na mipasuko ya kijamii.
Baadhi ya watoto
wametumbukizwa katika nyanyaso na dhuluma za kijinsia. Baadhi ya watoto
wametekwa nyara na wengine kupotea katika mazingira tatanishi. Afghanstan
inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliouwawa kutokana na mashambulizi
ya kivita. Mashambulizi ya kivita nchini Siria yamepelekea watoto zaidi ya 1,
854 kufariki dunia na wengine kupata vilema na majeraha ya kudumu.
Comments
Post a Comment