Mapadri kemeeni udhalilishaji wa watoto-Ask Msonganzila

Askofu wa Jimbo Katoliki  Musoma Michael Msonganzila akitoa Daraja Takatifu la Upadri kwa Shemasi Zedekia Mwinura katika Parokia ya Mawisenge Jimboni Musoma hivi karibuni (Picha na Veronica Modest)

Na Veronica Modest Musoma
ASkofu wa Jimbo Katoliki  Musoma Mhashamu Michael Msonganzila amewataka mapadri  kuhakikisha hawaoni aibu kukemea  vitendo  vyovyote vinavyodhalilisha watoto.
Askofu Msonganzila ameyasema hayo katika Ibada ya Misa Takatifu alipokuwa anatoa  Daraja Takatifu la Upadri kwa shemasi Zedekia Mwinura katika Parokia ya Mwisenge Jimboni humo.
Askofu Msonganzila amesema kuwa, Padri Zedekia anapata Upadri wakati Kanisa linakubwa na kashfa mbalimbali mojawapo ikiwa ubakaji na ulawiti wa watoto.
 “Ninapokupa Daraja hili Takatifu la Upadri katika mazingira haya tatanishi hakikisha unasimama imara katika kumshuhudia Kristo.
Ulimwengu unakumbwa na kasoro nyingi za rushwa, mauaji, kutokuwajibika manyanyaso ,na wakati mwingine inakatisha tamaa katika maisha yetu ,ila wajibu wetu una bakia palepale kuwa wewe ni kuhani,mchungaji, kayainjilishe maizngine hayo hivyo usione aibu kuyakemea na toa sauti ya kinabii”amesema Askofu Msonganzila.
Askofu Msonganzila   amewataka kuhakikisha wanatoa mafundisho yanayozungumzia umuhimu wa kumlinda mtoto,katika mazingira yote ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kwa kuwa Kanisa linalokuwa ni lazima liwe na watoto na watoto ndio mapadri,wazazi  na viongozi wa baadae.
 Akitoa neno la shukurani mbele ya Askofu Msonagnzila , Padri Zedekia Mwinura amemshukuru Askofu wa Jimbo la Musoma Michael Msonganzila kwa kukubali kumpatia daraja Takatifu la Upadri kwani lengo lake la kumtumikia Mungu kupitia Upadri limetimia na ilikuwa ni nia yake uya siku nyingi,na zaidi amemuahidi kuhaikikisha anayatekeleza yale yote aliyojifunza juu ya imani ya Kanisa Katoliki.
Padri Zedekia amewashukuru wote walioshiriki katika kuhakikisha siku yake ya kupewa daraja Takatifu la upadri inafika ,akiwa na afya njema kabisa lakini zaidi akiwa amejiandaa vema kuanza kukabiiliana na Utume mpya wa kuchonga kondoo wa Bwana popote atakapopangiwa.
Amewashukuru sana wazazi ,ndugu na jamaa zake kwa kukubali yeye apewe daraja hilo Takatifu licha ya changamoto za hapa na pale lakini anamshukuru Mungu changamoto hizo aliweza kuzivuka na hatimaye kufanikiwa kupokea daraja hilo Takatifu,na zaidi amewashukuru mapadri wa jimbo hilo kwa kumtia moyo pale alipoonekana kukata tamaa.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI