Magufuli: Uwezo wa miradi mikubwa tunao
RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania ina uwezo
mkubwa wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini pasipo na kutegemea
fedha zenye masharti zinazotolewa kutoka kwa wafadhili na wadau wa kimataifa wa
maendeleo.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la 3 la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi (Agosti 1, 2019), Rais
Magufuli alisema uzinduzi wa Jengo la Uwanja huo ni ushahidi wa wazi wa
usimamizi na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazotokana na kodi ya
wananchi.
Ameongeza
Jengo la Uwanja huo limejengwa kwa asilimia 100 kutokana na kodi za Watanzania,
na hivyo kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa
Barabara Nchini (TANROAD) kusimamia vyema miundombinu ya Uwanja huo kwa
kuhakikisha kuwa inatunzwa ili kuakisi vyema taswira ya Jiji la Dar es Salaam
na Watanzania kwa ujumla.
Kwa
mujibu wa Rais Magufuli jengo hilo litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya
abiria Milioni 6 kwa mwaka limeigharimu Serikali kiasi cha Tsh Bilioni 722
ambazo ni fedha zilizotolewa na Serikali, limeweza kuifanya Serikali kuaminika
na kuwa na udhubutu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kupitia fedha za ndani.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Serikali
itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya anga nchini, kwa kuwa sekta hiyo
imekuwa kiungo muhimu katika maendeleo ya sekta ya Utalii, kwani kila siku
takribani watu Milioni 12 duniani hutumia usafiri wa anga kutokana na kuwa njia
ya haraka na ya uhakika kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.
Akifafanua
zaidi Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoa
kipaumbele kwa makampuni ya kitanzania yanapewa nafasi katika maduka
yatakayofunguliwa ndani ya Uwanja huo ili kuwawezesha kufaidi matunda ya kodi
yao sambamba na kuweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi
Patrick Mfugale alisema tangu mwaka 2004-2011 Serikali imechukua hatua
mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya majengo ya Uwanja wa ndege
vyaJulius Nyerere ikiwemo ujenzi wa Jengo jipya la tatu la abiria katika uwanja
huo, kutokana na majengo ya sasa ya jengo la I na II kukabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa
kuhudumia abiria.
Anaongeza
kuwa ujenzi wa Jengo hilo la tatu la abiria lilisimama ujenzi wake mwaka 2016
kutokana na mkandarasi kudai Tsh Bilioni 29, ambapo awali alishapokea kiasi cha
Tsh Bilioni 380 kati ya Tsh Bilioni 560 zilizohitajika kwa ajili ya ukamlishaji
wa jengo hilo hapo awali, lakini mwaka 2017 Serikali ilitoa zabuni ya ujenzi wa
mradi huo kwa mkandarasi mwingine kutokana mkandarasi aliyepita kuwa na kasi
ndogo ya utekelezaji wa mradi.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Mfugale alisema kutokana na kasoro zilizojitokeza, shughuli
za ujenzi wa jengo hilo zilipelekwa kwa kampuni ya TECU na mshauri mwelekezi
kampuni ya Arab Contractor ambapo hadi kufikia Mei 29 mwaka huu zilikamilisha
ujenzi wa jengo hilo na kusubiri kukabidhiwa kwa Serikali kwa ajili ya kuanza
kutumika kwake.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mhandisi Julius
Ndyamukama alisema hadi kufikia sasa jumla ya makampuni 18 kati ya 23 ya
kimataifa tayari yamehamishia shughuli zao katika Uwanja huo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za usafiri
kwa abiria wanaosafiri kwenda nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa katika kuimarisha usimamizi bora wa Jengo la Uwanja huo, Mamlaka hiyo pia
imewapatia mafunzo watumishi wake kwa ajili ya kupata uelewa wa pamoja wa namna
bora ya kulinda miundombinu ya Uwanja huo na hadi sasa imepokea Tsh Milioni 500
kutoka Serikalini ilizozilipa kwa mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kwa ajili
ya kutoa mafunzo hayo.
Comments
Post a Comment