DC Songwe apongeza utendaji wa Askofu Nyaisonga
MKUU
wa Wilaya ya Songwe,Samwel Jeremiah amemuelezea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya,Mhashamu
Gervas Nyaisonga kuwa ni mtu wa aina
yake ambaye amejawa hekima na busara
katika uchungaji wake.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo
alipokuwa mgeni rasmi katika
mahafali ya tisa ya kuwaaga wahitimu
wa mafunzo ya Uuguzi na
Ukunga katika ngazi ya stashahada katika
Chuo cha Mwambani, kilichopo Kata ya Mkwajuni, wilaya ya Songwe, mkoani Songwe.
“Kwa kweli
nimemshangaa na kumuona ni kiongozi wa
ajabu na nilikuwa nikimsikia na leo nimejionea nilipoambiwa kuwa yeye Askofu
Mkuu amekataa kuwa mgeni rasmi na
kupendekeza lazima awe Kiongozi wa Serikali...
Nilijiuliza sana kwamba kwanini Baba Askofu amefanya
hivyo...nikasema Baba amejawa na unyenyekevu, hekima na busara za pekee,”anasema Mkuu wa wilaya hiyo na
kuongeza;
“Niseme tu Baba Askofu leo umenipa heshima kubwa sana kuwa mgeni rasmi wa tukio hili . mahafali ya
leo yakabadilishe maisha ya wauguzi na wakunga wote, nimeambiwa kuwa
chuo hiki.”
Hata hivyo amewataka
wahitimu kuondoa hofu juu ya
ajira kwani serikali ya awamu ya tano
inatoa kipaumbele kwa sekta ya afya.
“Niwaambie tu kuwa kuna
hospitali zaidi ya 67 na vituo vya afya
zaidi ya 350 vinajengwa nchi nzima vyo hivi
vikikamilika vinahitaji wahitimu
kama ninyi mkafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kuliletea sifa Kanisa,” amesema.
Kwa upande wake Askofu Mkuu
Gervasi Nyaisonga amewasihi
wahitimu hao ambao wameapa kiapo cha utii kama alivoapa mwanzilishi wa fani ya uuguzi
duniani Florence Nightngale kuwa
kielelezo ya maisha yao katika utume
wao na wanapoishi.
“Naomba kiapo kile kiwe kwa vitendo kule muendako,mkafanye kazi
kama mlivyofundishwa kwa bidii, kwa uaminifu na kwa umakini wa hali ya juu
ukumbuke kuwa unayemhudumia ni binadamu kama wewe , fanya kazi huku
ukimuhusisha Mungu katika kazi zako,” amesema Askofu Nyaisonga.
Askofu Nyaisonga amesema Serikali inayo mkono mrefu, inayo nguvu
na ndiyo imepewa dhamana na Mwenyezi
Mungu kusimamia rasilimali za Nchi,kwa hali hiyo hatuna namna na hatuwezi kufanya chochote bila kuitegemea
serikali vinginevyo tutaendelea kushirikiana nanyi na hatutachoka kuja kuwaona
kuomba ushauri na misada ya namna mbalimbali.
Kwa upande wake Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, victoria
Mwakigili alipigilia msumari kuhusu suala la mavazi ambayo wanapaswa kuvaa wauguzi ikiwemo kutumia lugha nzuri kwa
wagonjwa.
Comments
Post a Comment