Kila mwandamu ampe Mungu nafasi ya kwanza – Ask.Ruzoka

Na Thomas Mambo-Tabora.

SHemasi na Waamini wahimizwa daima kumruhusu Kristo kutawala katika maisha yao sambamba na kuwa na moyo wa Shukrani kwa Mwenyezi Mungu mpaji wa vyote.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo kuu Katoliki Tabora katika Misa Takatifu ya Ushemasi   kwa Frateri Patrick Bergin   katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimboni Tabora.
Aidha Askofu Ruzoka amemuasa Shemasi Bergin daima awe na Ibada kwa Mama Bikira Maria Mama wa Kanisa na Mama wa Mapadri ili aweze kudumu katika maisha yake mapya ya utumishi katika Kanisa la Kristo.
Akitoa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu Tabora, Askofu Ruzoka amesema kila mkristo hana budi kuutafuta kwanza ufalme wa Mbinguni na megine yote atayapata kwa ziada.
Amempongeza Shemasi Patrick kwa uamuzi wake wa busara nakusema kila mwandamu lazima ampe Mungu nafasi ya kwanza, ili baada ya maisha haya aweze kuuona ufalme wa Mungu ambao kila mmoja wetu anautamani kuufikia.
Zoezi hilo la kiroho litafanikiwa tu pale kila mmoja atatekeleza wajibu wake hapa duniani, na ndipo siku mmoja ataungana na Kristo katika uzima wa milele ambao mwanadamu anaitiwa ,ili aufikie hanabudi kujiamisha kwa Kristo Yesu kwauaminifu mkubwa.
Shemasi Patrick Joseph ni mzaliwa wa Nchi ya Marekani, amezaliwa mwaka 1964. Amemaliza Masomo huko marekani katika Chuo Kikuu cha “Undergraduate St.John College” katika mji wa Annapolis, katika Jiji la Maryland.
 Pia amesoma shahada ya uzamiri katika Chuo Kikuu cha IIIinois, pia amesomea Shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha East Anglia, Norwich Uk.
kwa sasa anaendelea na masomo yake ya Teolojia katika Chuo Kikuu cha Union Chicago IIIinois.
 Yeye ni mtoto wa nne kati ya watoto tisa, wazazi wake ni James Bergin na Angela Gould.
 Shemasi Patrick Joseph anatarajia kupokea Daraja Takatifu ya UpadriApril  18 mwaka 2020 huko Marekani, na baadae kurejea Jimboni Tabora kufanya utume wake kama Padri mwanajimbo.
Misa hiyo ya Ushemasi ilihudhuriwa na ndugu wa Shemasi Patrick kutoka nje ya Nchi, Mapadri , watawa na waamini wa Jimbo Kuu Tabora.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI