WASIFU WA MAREHEMU PADRI UBALDUS KIDAVURI



A. ALIPOZALIWA NA KULELEWA

·      Alizaliwa  tarehe 13. 10.1961 katika  parokia ya Kisangara Juu  katika wilaya ya Mwanga, jimbo Katoliki la Same
·      Wazazi wake ni  Baba Francis Maliare na Mama Odilia Odilo
·      Alipata Sakramenti ya Ubatizo tarehe 31.10.1961 katika parokia ya Kisangara Juu
·      Alipata Sakramenti ya Kipaimara tarehe 31. 08.1974 katika parokia ya Kisangara Juu

B.   ELIMU YAKE

·      Alisoma shule ya Msingi Kiasangara Juu  darasa la kwanza hadi la saba na  kuhitimu tarehe 04.10.1975
·      Alipata elimu ya Sekondari katika Seminari ya Mt. Petro Morogoro  na kuhitimu Kidato cha nne  tarehe 21/11/1980.
·      Baadaye alijiunga na seminari ya Mt. Yakobo Kilema Moshi kwa ajili ya Masomo ya Kidato cha tano na sita ambapo  alihitimu tarehe 7.4. 1983.
·      Alijiunga na seminari Kuu ya Mtakatifu Bikira Maria wa Malaika Kibosho Moshi kwa ajili ya masomo ya Falsafa  tangu tarehe 31 /7/1983 hadi tarehe 11/6/1985.
·      Mwaka huo huo wa 1985 aliendelea na masomo ya Tauhidi  katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga mpaka 1990.

·      Alipata daraja la Ushemasi tarehe 18.6. 1992
·      Alipata Daraja la Upadri  tarehe 17/12/1992



C.         UTUME WAKE JIMBONI
·      Desemba  1992- Mlezi  Dido Chuo cha Malezi
·      Desemba 1992  Kaimu Paroko- Parokia ya Chanjale/ Kapelano Kisekibaha
·      Mwaka 1993-1998 alikuwa paroko wa parokia ya Ugweno
·      Mei – Novemba  1998  alitumwa kusomea mawasiliano katika Chuo cha Uandishi wa  Habari- Ndola Zambia
·      1998 -1999 Alikuwa paroko wa parokia ya  Chabaru

  

D.   UTUME WAKE KATIKA BARAZA LA MAASKOFU

·      Aliteuliwa  na  Kamati ya  Tendaji  ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania  ( Permanent Council) tarehe 7.11.2003  kuwa  mhariri mkuu wa Gazeti la Kiongozi, Mratibu wa programu  ya radio na TV. Alianza kazi rasmi mwezi Desemba 2003  katika Idara ya Mawasiliano.
·      Baadaye mwaka 2007 alitumwa huko Roma nchini Italia kujiendeleza katika fani ya Mawasiliano katika Chuo cha Msalaba Mtakatifu ambapo mwaka 2010 alihitimu shahada ya uzamili (Masters Degree) katika Mawasiliano. Wakati wa Masomo yake Roma alikuwa mhariri wa programu ya Kiswahili Radio Vatican 2007 mpaka 2009
·      Baada ya masomo yake Roma alirudi jimboni Same na mwaka 2011 alitumwa kuwa paroko wa parokia ya Ugweno.
·      Aliteuliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tarehe 1. 7.2012 kuwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Walei na akateuliwa  tena tarehe 1 Julai 2016 kuendelea na utume huo. Mpaka mauti yalipomkuta alikuwa anaendelea na utume huo.
E : UGONJWA WAKE:
Alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Moyo ambao ulisababisha kifo cha ghafla tarehe 13/04/2018
F:  SHUKRANI
Baraza linashukuru kwa  Mababa Askofu , mapdri na watawa na Wakristo mbali mbali ambao wameshiriki kwa njia  mbali mbali kutoa faraja kwa Jumuiya ya Sekretariati tulipopatwa na msimba huu mzito.





Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU