MTAKATIFU WA SIKU

MTAKATIFU MARKO MWINJILI NA MTAKATIFU
EUFRASIA PALLETIER, MTAWA


Leo Mama Kanisa anamkumbuka na Kumheshimu Mtakatifu Marko Mwinijili wa (Karne ya Kwanza) na Mtakatifu EUFRASIA PELLETIER Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika.

Mtakatifu Marko Habari za kale zinasimulia kuwa Mtakatifu Marko alikuwa Binadamu ya Mt. Barnaba na mmoja wa Wanafunzi waliomfuata Yesu Kristo. Lakini Mtakatifu Epifani anatuhadithia kuwa Mtakatifu Marko na wenzake walikataa kusadiki kwanza walipo ambiwa na Bwana wetu maneno haya . “

 Msipokula mwili wa mwana na mtu, msipokunywa damu yake hamtakuwa na uzima ndani yanu”.
Mtakatifu Petro alimuongoza Marko kisha kufufuka kwake Bwana wetu, akamfanya kama mwandishi wake. injili iliyoandikwa na Marko ni kama jumla ya mafundisho yalimofundishwa na wakuu wa mitume ,hata walimu wakanisa husema ni Injili ya Mtakatifu PETRO. Marko ametusimulia habari nyingine zisizo andikwa katika Injili nyingine, kama vile sifa ya yule mjane masikini aliyetoa sadaka yake hekaluni. Ni yeye aliehubiri injili huko Aleksandaria (Misri), na ndivyo alivyo anza kuongoza nchi ya Misri kwa Ukiristu. Pia alimsindikiza Mt. Paulo katika safari yake yakwanza na alimfuata huko Roma (Italia). Alikufa kama shahidi , na mwili wake umezikwa katika Kanisa la san marko huko Venesia (Italia).

Tarehe hiyo hiyo Aprili 25
Kanisa linakumbuka Mtakatifu Eufrasia Pelletier Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika
Alizaliwa katika kisiwani kidogo huko Ufaransa , Wazazi wake walimpa jina la Rosa Virginia. Alipokuwa na umri wa miaka Kumi na mInane, aliingia utawa akapata jina la Sista Eufrasia. Alianzisha Shirika la mchungaji mwema. Masista hawa wanashugulikia na kuwasaidia wanawake wanao zaa watoto nje ya ndoa . Eufrasia alikuwa Kiongozi wa Shirika kwa muda wa miaka Thelathini na Mitatu, akajenga Konventi Mia Moja na Kumi katika nchi mbalimbali. Mtakatifu Eufrasia alifariki mwaka 1868, na akatangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1940.

Haya ndio maisha ya Watakatifu Mtakatifu Marko Mwinijili wa (Karne ya Kwanza) na Mtakatifu Eufrasia Pelletier Mtawa na Mwanzilishi wa Shirika, kwa mujibu wa kitabu cha Watakatifu.

WATAKATIFU WOTE WA MUNGU MTUOMBEE

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU