DC Geita aunga mkono matamko la maaskofu
Na Marco Kanani, Geita
Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi amesema anaunga
mkono Waraka wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki katika kipindi cha Kwaresima
akisema kuwa, una sauti ya kinabii.
Amesema hayo wakati akitoa salamu Misa Takatifu
ya Mkesha wa Pasaka jimboni Geita amabyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki
Geita Mhashamu Flavian Kassala.
“Binafsi amaejitahidi kuusoma kwa makini waraka
huo wa Maaskofu na sikuona chochote kibaya katika waraka huo kwani yote yaliyomo
ni mema sana.
Mimi niseme tu kuwa, mti wowote ambao ni mgumu
kama hautaki kupinda wenyewe ukilazimishwa ama kupindishwa na upepo hautabaki
salama lazima utavunjika hivyo sisi kama serikali tuko tayari kujirekebisha
pale ambapo tunakosea, "amesema DC Kapufi.
Amesema, anachojua yeye ni kuwa kabla ya
Maaskofu hawajaandika waraka wanasali kwanza na kumshirikisha Mungu mawazo yao,
hivyo wakitoa neno linakuwa na upako wa kimungu na hivyo nyaraka zao zimejaa
maono matakatifu.
Comments
Post a Comment