Askofu Mkuu Protas Rugambwa akitoa Daraja Takatifu la Upadri kwa mashemasi wawili jimboni Kigoma (Na Mpiga picha wetu). Mapadri wapya wa Jimbo Katoliki Kigoma wakitoa baraka kwa Askofu Joseph Mlola ALCP/OSS (Wa kwanza waliopiga Magoti) na Askofu Mkuu Protas Rugambwa baada ya kupata Daraja Takatifu la Upadri hivi Karibuni (Na Mpiga Picha wetu).
Posts
Showing posts from August, 2019
DC Songwe apongeza utendaji wa Askofu Nyaisonga
- Get link
- X
- Other Apps
Na Thompson Mpanji, Songwe MKUU wa Wilaya ya Songwe,Samwel Jeremiah amemuelezea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya,Mhashamu Gervas Nyaisonga kuwa ni mtu wa aina yake ambaye amejawa hekima na busara katika uchungaji wake. Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tisa ya kuwaaga wahitimu wa mafunzo ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya stashahada katika Chuo cha Mwambani, kilichopo Kata ya Mkwajuni, wilaya ya Songwe, mkoani Songwe. “Kwa kweli nimemshangaa na kumuona ni kiongozi wa ajabu na nilikuwa nikimsikia na leo nimejionea nilipoambiwa kuwa yeye Askofu Mkuu amekataa kuwa mgeni rasmi na kupendekeza lazima awe Kiongozi wa Serikali... Nilijiuliza sana kwamba kwanini Baba Askofu amefanya hivyo...nikasema Baba amejawa na unyenyekevu, hekima na busara za pekee,”anasema Mkuu wa wilaya hiyo na kuongeza; “Niseme tu Baba Askofu ...
Kardinali Pengo afanya ziara ya kichungaji Shinyanga
- Get link
- X
- Other Apps
N a Natoly Salawa ±Shinyanga ASkofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka mapadri kuambatana daima na Kristo katika utume wao badala ya kujiambatanisha na malimwengu. Kadinali Pengo ameyabainisha hayo katika Kanisa Kuu Mama Mwenyehuruma Ngokolo Shinyanga wakati wa mahubiri yake katika adhimisho la Ekaristi Takatifu na utowaji wa Daraja Takatifu la Upadri kwa mashemasi sita katika sherehe ya Kupalizwa Mbinguni Bikira Maria iliyofanyika 15 Agosti, 2019. Katika ujumbe wake,Kadinali Pengo amewataka mapadri hao wapya kwenda kufanya utume wao kwa uaminifu huku wakitambua kuwa upadri ni kujitoa sadaka kwa Mungu, hivyo wasifanye utume wao kinyume na matarajio ya Wakristo ambao wanamategemeo makubwa juu yao na badala yake wamtangulize Kristo katika huduma yao kwa Kristo na Kanisa lake. Aidha Kadinali Pengo ametoa wito kwa waamini wa jimbo Katoliki Shinyanga kuendelea kuwaombea mapadri wapya na mapa...
Kila mwandamu ampe Mungu nafasi ya kwanza – Ask.Ruzoka
- Get link
- X
- Other Apps
Na Thomas Mambo-Tabora. SHemasi na Waamini wahimizwa daima kumruhusu Kristo kutawala katika maisha yao sambamba na kuwa na moyo wa Shukrani kwa Mwenyezi Mungu mpaji wa vyote. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo kuu Katoliki Tabora katika Misa Takatifu ya Ushemasi kwa Frateri Patrick Bergin katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimboni Tabora. Aidha Askofu Ruzoka amemuasa Shemasi Bergin daima awe na Ibada kwa Mama Bikira Maria Mama wa Kanisa na Mama wa Mapadri ili aweze kudumu katika maisha yake mapya ya utumishi katika Kanisa la Kristo. Akitoa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Terezia wa Mtoto Yesu Tabora, Askofu Ruzoka amesema kila mkristo hana budi kuutafuta kwanza ufalme wa Mbinguni na megine yote atayapata kwa ziada. Amempongeza Shemasi Patrick kwa uamuzi wake wa busara nakusema kila mwandamu lazima ampe Mungu nafasi ya kwanza, ili baada ya maisha haya aweze kuuona ufalme wa Mungu ambao kila mmoja wetu anau...