‘Bila ushirikiano wa Serikali na Kanisa hakuna maendeleo’
Na Izack Mwacha Singida ASKOFU wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda, ameipongeza serikali ya Mkoa wa Singida, kwa kutoa ushirikiano na Kanisa katoliki katika shughuli za maendeleo. Askofu Mapunda ameyasema hivi karibuni katika uzinduzi wa miaka 22 ya Radio Maria Tanzania iliyofanyika Parokia ya moyo Mtakatifu wa Yesu Jimbo Katoliki Singida. Katika homilia yake Askofu Mapunda amesema kuwa ushirikiano ukidumishwa Kati ya serikali na Kanisa ni lazima maendeleo yawepo,kwani miongoni mwa mambo ambayo yanaleta chachu ya Nguvu, umoja na mshikamano ni ushirikiano ambao kwa kiasi kikubwa unaleta hali ya kujaliana, hivyo anategemea maendeleo makubwa zaidi katika Jimbo la singida Askofu mapunda amesisitiza kuwa, ili imani ya Kanisa Katoliki iendelee kudumu zaidi ni lazima kwa kila mkristo mkatoliki mmbatizwa afahamu umuhimu wake wa kuchangia vyombo vinavyoweza kuisambaza injili hiyo kwa kasi zaidi ulimwenguni kote ikiwemo Radio Maria, kwani hiyo ni njia pekee amb...