Kahama wafanya harambee kujenga Chuo cha Ukatekista
Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama
Mhashamu Ludovick Minde ametoa wito kwa waamini kuziheshimu alama mbalimbali za
imani ndani ya Kanisa.
Askofu Minde alitoa wito huo katika homilia
aliyotoa katika Misa Takatifu iliyoiadhimisha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu
Karoli Lwanga, Parokia ya Kahama mjini
ambapo pia kulikuwa na harambee ya kuchangia ujenzi wa Chuo cha
Makatekista jimboni hapa.
Akiongea katika misa hiyo
aliwataka waamini kuheshimu alama mbalimbali
za imani ndani ya kanisa katoliki
kuanzia na Msalaba Mtakatifu ambayo ndiyo ishara kuu ya Mkirsito Mkatoliki.
Askofu Minde amesema waamini
waache kuona aibu kuwa na Msalaba kuweka katika nyumba zao , biashara na Rozali
, kusoma Bibilia , maji ya Baraka
katika familia zetu hizo ndiyo baadhi ya alama ya Mkatoliki lazima tuzionee
fahari.
Amesema katika maisha ya imani
lazima waamini waendelee kumkumbatia Yesu Kristo , kusoma neno la Mungu ,
kusali katika familia , jumuiya ndogondogo
na kuhudhulia Misa Takatifu.
Askofu Minde amesema anawapongeza
Mababa Mapri , Watawa kwa kazi nzuri wanayofanya katika malezi ya kuwalea
waumini kiroho na kutaka kuendelea
kumuomba Mungu aendelee kutujalia imani.
Mmoja kati ya waliokuwa wageni rasmi katika
harambee hiyo, Frederick John akiongea
baada ya misa alisema anampongeza sana, Askofu Minde kwa kuona umuhimu wa
kujenga chuo cha Makateksta ambao ni wa
muhimu sana katika mafundisho ya imani ya Kanisa.
John amesema katika kipindi hiki
cha sayansi na teknolojia , Makatekista wanapaswa kujengewa uwezo wa kutosha
kutakako wasaidia kuweza kufundisha
vizuri katekismu ya kanisa katoliki.
Amesema mafundisho ya makatekista
ndiyo chimbuko la imani pamoja na miito
ya kwenye ndoa, upadri na utawa ndani ya kanisa , kwa hiyo kukamilika kwa chuo hicho mwishoni mwa mwaka huu kitawasaidia sana
kuwajengea uwezo walimu hao wa dini.
Comments
Post a Comment