Ask Msonganzila aonya juu ya migogoro katika familia
askofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila amesema migogoro ya mara kwa mara,wizi na kiburi ni kutokana na waamini kujisahau
kuwa wameumbwa kwa mfano wa Sura ya Mungu na hivyo kufanya vitu visivyoendana
na tabia za Mungu.
Askofu
Msonganzila ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kichungaji katika Parokia ya
Kigera ambapo alitembelea kigango cha Buruma na kubariki Kanisa jipya na
kufungua jiwe la msingi.
Akiwa
katika kigango cha Bisumwa alibariki msingi wa Kanisa kubwa lenye uwezo wa
kuchukua waamini zaidi ya 1500 kwa
wakati mmoja na kutoa Sakaramenti ya Kipaimara kwa waamini zaidi ya 390 katika
Parokia hiyo.
“Wizi
unatoka wapi, kutokuwajibika mahali pa kazi kunatoka wapi nataka moyo
unaokujika moyo wa unyenyekevu, unaobondeka na kukunjwa kwa neno la Mungu dunia
yetu tunaifahamu ilivyo kwa sasa watu tumejaa kiburi,hakuna nidhamu kwa
wazazi,hakuna utii kati yenu ninyi wenyewe
Hii
sura ya Mungu tunaipeleka wapi kwa nini mapigano kila mara, katika familia
hakuna utulivu na watoto wanajifunza nini kutoka kwenu wazazi,hata majirani
hatukai nao kwa amani, tuheshimu sura hiyo,”amesema Askofu Msonganzila.
Amewataka vijana waliopata sakramenti ya
Kipaimara kuhakikisha wanakuwa waalimu na wahusika wa kusikiliza na
kushikiria neno la Mungu kikamilifu kwa
matendo na majitoleo katika kufanya kazi ya Mungu, na kutokuruhusu kupotoshwa
imani yao ya Kanisa Katoliki,kwani vijana wengi wamekuwa wakipotoka kwa kuhamia
makanisa mengine na kuacha imani yao waliyobatizwa na kupokea sakramenti zote
za awali.
Amewapongeza waamini wa Parokia hiyo kwa
kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele mbali ya changamoto mbalimbali za
maisha wanazokumbana nazo,ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maeneo yote ya Kanisa
wanatunza kumbukumbu vizuri kwa ajili ya faida yao na kizazi kijacho ,ili kuondoa migogoro ya ardhi
ambayo inaweza kuibuka hapo baade.
Paroko wa Paroki hiyo Padri Robert Luvakubandi
amesema ziara ya Askofu wa Jimbo la Musoma katika Parokia yake itasaidia sana
kuimarisha waamini kiroho na hata kuwaongezea nguvu ya imani wale ambao
walikuwa wanataka kulegea na kurudi yuma kiimani.
Paroko
huyo aliwapongeza waamini wa kigango cha Buruma,Bisumwa na Parokia ya Kigera
kwa ushirikiano wao mzuri wanaounyesha katika kukua kiimani, hasa katika
ushiriki wao wa ujenzi wa makanisa
unaoendelea katika maeneo yao kwa kuwa wamejitoa kwa hali na mali katika kutoa
michango yao ya kifedha na nguvu kazi.
Comments
Post a Comment