Askofu Ruwa’ichi: Msiabudu mali
waamini nchini
wametakiwa kuacha kuabudu mali zao kama vile biashara, mashamba, ofisi,mifugo
mazao nk. badala yake wamwabudu Mungu pekee mtoaji wa vyote.
Hayo
yamesemwa na Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam
Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi
wakati wa homilia yake hivi karibuni katika Jubilee ya Miaka 50 ya
Updri ya Padri Camille Neuray Paroko wa Parokia ya Mt.karoli Lwanga Yombo Dovya.
“Kinacho
tutunza sio mali, bali ni Mungu mwenyewe anaye sitawisha mali na kuzifanya zizae. Hivyo tunapaswa
kumwabudu Mungu na sio kitu kingine chochote,” amesema.
Amesema kuwa adhimisho la jubilee ni jambo
linalobeba maana kadhaa miongoni wa
mambo hayo ni fursa ya kumshukuru Mungu,
kujiweka wakfu upya, kujiaminisha kwake tena kujinyenyekesha na kuomba
toba pamoja na neema na baraka.
Hata hivyo
Amesema kuwa watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwa kama akina Paulo, Adrea ,
filipo na wengine waliokuwa mitume wa Yesu kama sehemu ya kuiita miito
mitakatifu katika jamii wakiwemo vijana na watoto kuingia katika wito wa utawa
Kama Padri Camille Naeuray.
Aidha
adhimisho hilo ni ungamo lakiimani kana kwamba bila Mungu hatufanikishi kitu
hivyo wanapaswa kumuomba Mungu ili awasaidie kufanikisha kazi aliyowaitia
katika wito wa kumtumikia Mungu hapa ulimwenguni.
Askofu
Ruwa’ichi amempongeza Padri Camille Neuray katika uaminifu wake wa kudumu
katika utume na kujitoa sadaka katika kufanya utume bila kujibakiza.
Pamoja na kumuombea kila la heri ili aweze kufikia
Miaka 50 ya Utume.
Padri
Camille Neuray wa Shirika la Wakamilian alianza utume wake wa Upadri katika
Parokia ya Ngerengere Mkoani Morogoro, Kisha Mt Camillian Kiwalani Dar
es sala kwa sasa anaendelea na utume huo katika Parokia Mt.Kaloli Lwanga -Yombo
Dovya.
Misa hiyo ya
jubilei ya miaka 50 ya updri wa padri Camille Neuray kutoka Parolika ya Mt.
Karoli Lwanga Yombo Dovya imeongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thadeus
Ruwa’ichi akishirikiana na Monsinyori Mbiku na mapadri wa shirika la wakamilian
pamoja na mapadri wa mashirika mengine na mapadri wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es
salaam.
Comments
Post a Comment