MAHAKAMA YA MAFISADI RASMI JULAI

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amebainisha kuwa sasa mahakama rasmi ya mafisadi itaanza kazi Julai mwaka huu.
Akiongea mkoani Geita katika Misa Takatifu ya kumsimika na kumweka wakfu Askofu Flavian Kassala Jimbo la Geita hivi karibuni,waziri mkuu amesema sasa wote wanaoendekeza vitendo vya ufisadi kiama chao kimefika.
Kassim Majaliwa amesikitika kuona mafisadi wanasababisha wananchi wasio na hatia kuteseka na wakati mwingine kupoteza maisha kutokana na mafisadi wachache wasio na huruma wala utu kutumia nafasi walizonazo kujinufaisha.
Amesema kanisa limefanya jitihada kubwa kujenga jamii yenye amani,upendo na kuthamini utu lakini bado tatizo la ufisadi limeendelea.
Amelipongeza kanisa na kuliomba liendelee kuipa serikali ushirikiano katika vita hiyo kama linavyofanya katika utoaji wa huduma za kijamii.
Waziri mkuu Majaliwa licha ya kusema kanisa linaongoza nchini katika kutoa huduma za kijamii,amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili huduma hizo ziendelee kuinufaisha jamii.
Mahakama ya mafisadi inaaminika kuwa kwa kiwango kikubwa itasaidia kulimaliza tatizo la rushwa nchini.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU