HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU
Na Philip Komba
Utangulizi: Ibada ya Moyo Mtakatifu
wa Yesu ni moja ya ibada zinazojulikana sana katika Kanisa Katoliki. Ibada hii
inauona Moyo wa Kibinadamu wa Yesu kama mwakilishi wa Mapendo yake ya Kimungu kwa wanadamu, na Kanisa nayo inaiona kama
Mapendo na Huruma ya Yesu kwa wanadamu wote.
Ibada
ya Moyo Mtakatifu wa Yesu imefikia hatua hii tunayoishuhudia leo kutokana na
maelekezo ya Mtakatifu Margareta Maria Alakok aliyejifunza uendelezaji wake
wakati alipokuwa anatokewa na Yesu kwa mfululizo kati ya mwaka 1673 na mwaka
1675.
Mtawa
mwingine tena, Mwenyeheri Maria wa Moyo Mtakatifu (1863-1899), kutoka Chama cha
Kitawa cha Mchungaji Mwema huko Ujerumani, aliisisimkia sana ibada hii baada ya
kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Yesu na akawahi hata kumwomba Papa Leo
XIII, autolee ulimwengu wote kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu kama alivyotumwa na
Yesu.
Wakati
wa kipindi cha enzi ya kati, watangulizi wa ibada hii mpya, walijitokeza kutoka
sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kanisa Katoliki na kuifanya ishike kasi na
kujulikana sana katika Kanisa hilo.
Asili ya Ibada: Ibada
ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni maendelezo ya Ibada ya ‘Ubinadamu Mtakatifu wa
Kristo.’ Uhuishaji wa maisha ya Kitawa na ari ya Mtakatifu Bernard wa Klervo na
ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi katika Karne ya 12 na 13, pamoja na shauku ya
wapiganaji wa vita vya Msalaba waliorudi kutoka Nchi Takatifu, walianzisha
Ibada ya Mateso ya Kristo hasa ya Vidonda vyake Vitakatifu na zaidi sana lile
donda la Ubavuni mwa Yesu.
Ibada
hii ya Mateso ya Kristo ilishughulikiwa zaidi na vikundi vya Kitawa vya
Wafransiskani ikishabikiwa sana na Mtakatifu Bonaventura pamoja na Mtakatifu
Jean Eudes (1602 -1680). Kwa asili,
kulikuwa na ibada mbili zilizoungana, ibada ya Moyo Safi wa Maria, na nyingine
ya Moyo wa Yesu. Lakini polepole, ibada hizi mbili zilitenganishwa na tarehe 31
Agosti, 1670 kwa mara ya kwanza kabisa kulikuwa na sherehe ya pekee ya Moyo
Makatifu wa Yesu katika shule ya Seminari ya Rennes huko Ufaransa.
Watakatifu wanaohusiana na Moyo
Mtakatifu wa Yesu:
Mtakatifu Lutgarda (1246):
Vyanzo vya kihistoria ya Kanisa, vinasema kuwa Yesu alimtokea Lutgarda na
akamwambia amwombe neema yoyote aitakayo. Yeye akaomba uelewa wa lugha ya Kilatini ili asaidiwe katika
kuyaelewa maandiko.Akapewa, lakini aliona bado anakosa kitu. Akamwomba Yesu
wabadilishane mioyo. Yesu akakubali na kuanzia hapo Lutgarda alikuwa na ibada ya pekee kwa Moto
Mtakatifu wa Yesu.
Mtakatifu Mektildis Mkubwa (1298):
Yesu alimtokea na akamwamuru Mektildis ampende na aupende moyo wake katika Sakramenti
ya altare; naye akafanya kama Yesu alinyokuwa amemwamuru. Mtakatifu huyu
alikuwa kati ya wale wa kwanza kabisa kuwa na ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Mtakatifu Margareta Maria Alakok (1647-1690): Kama
ilivyokwisha kudokezwa Margareta Maria
Alakok ndiye aliyekuwa mwelekezi wa ibada hii na kuifanya kama ilivyo sasa.
Maelekezo kuhusu upokeaji wa Komunyo, Ibada ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi ,
kuabudu Ekaristi Takatifu kwa saa moja
kila siku ya Alhamisi, na kusherehekea sikukuu ya Moyo Mtakatifu yalikuwa baadhi
ya maelekezo ya Margarata Maria Alakok.
Estelle Faquette: Alipewa
Skapulari ya Moyo Mtakatifu wa Yesu tarehe 9/9/1876 na Mama Bikira Maria na
akaruhusiwa na Askofu wake Mkuu kutengeneza nyingi zaidi na kuwagawia waamini
wengine ilipofika tarehe 12/12/1876.
Mwenyeheri Maria wa Moyo Mtakatifu
(1863-1899): Tarehe 10/6/1898 Maria alipewa ujumbe
na Yesu wa kumpelekea Papa Leo X111 kumwambia autolee ulimwengu wote kwa Moyo
Mtakatifu wa Yesu. Kwa kuwa Papa hakuutilia maanani ujumbe ule wala
hakuuamini, tarehe 6/1/1889 alipelekewa ujumbe mwingine tena wa kumwambia kuwa
Ijumaa za Kwanza za kila mwezi ziwe kwa ajili ya Ibada ya Moyo Mtakatifu wa
Yesu. Tarehe 9/6/1899 Papa Leo
akatekeleza maagizo ya kuutolea ulimwengu wote kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Kibali cha Kipapa: Baada
ya kifo cha Margareta Maria Alakok, mashirika ya Kitawa tu ndiyo yaliyoruhusiwa
na Roma kuadhimisha misa maalum kwa heshima ya Moyo Mtakatifu wa Yesu. Lakini
kuanzia mwaka 1856, Papa Pius 1X aliiruhusu Kanisa Katoliki kwa jumla
kuadhimisha misa maalum kwa heshima ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Papa
Pius X aliamuru ile ibada ya kuutolea ulimwengu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu
iliyofanywa kwanza na Papa Leo X111 irudiwe kila mwaka. Papa Pius X1, katika
Waraka wake wa Kipapa wa tarehe 8 Mei, 1928 akiri kuwa ni kweli Yesu alikuwa
amejidhihirisha mwenyewe alipomtokea Margareta Maria Alakok na kutoa ahadi za
neema kwa wale watakaouheshimu moyo wake. Waraka wa Papa ulikuwa unarudia tena
na tena yale mazungumzo kati ya Yesu na Mtakatifu Margareta yakithibitisha
umhimu wa kuuheshimu Moyo huo wa Yesu kwa fidia ya dhambi zetu.
Siku
ya kumbukumbu ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
iliyozinduliwa na Papa Pius IX, Papa Pius X11 aliwaeleza Wakatoliki wote kwa
kinaganaga sana kuhusu ibada hii katika Waraka wake wa Kipapa wa tarehe 15 Mei,
1956.
Ukosoaji kuhusu utoaji heshima kwa
Moyo Mtakatifu wa Yesu: Wakristo wa madhehebu ya Kiorthodoksi
ya Mashariki wanaikosoa ibada hii wakisema kuwa imeuweka mno Moyo wa Yesu
isivyostahili katika hali ya ubinadamu. Papa Pius X11 katika moja ya Barua zake
aliujibu ukosoaji huo kwamba Moyo Mtakatifu wa Yesu unaheshimiwa kwa mujibu wa
Nafsi Takatifu ya Neno la kudumu milele na pia kama alama ya mapendo yake
inayoonekana ambayo ni ushahidi wa wokovu wetu.
0754
054 004 kwa msaada wa mtandao.
MOYO MT. WA YESU KRISTO WA NAZAZRETH NI UKAMILIFU WA MAPENDO YA MUNGU BABA
ReplyDeletetumwendee Yesu wa Huruma by Aloisius Daniel Ukweli utaponya majeraha ya jamii ya kikristo na jamii nyingine,Yesu anasisitiza TUWE WAKWELI ,TUISHI UKWELI,TUWAPE WATU UKWELI ILI WAUISHI UKWELI amina kwa jina la Yesu Mwana wa Mungu aliye hai.