MAANDALIZI YA KONGAMANO LA EKARISTI YAMEKAMILIKA

 ASKOFU MSAIDIZI wa Jimbo la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini akiongea na waandishi wa habari mapema leo juu ya kongamano la tatu la kitaifa la Ekaristi Takatifu jiji Mwanza.
yupo katikati Pichani.kushoto  ni Padiri - Titus Ngapemba - Katibu wa habari jimbo kuu la Mwanza na kulia ni Bernard James – Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano TEC.








 Sehemu ya wanahabari





Usiache kufuatilia maelekezo ya kiongozi huyo kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuanzia sasa lakini kikubwa ni kwamba.

Baraza la maaskofu Tanzania Tec limesema vita dhidi ya mauji,manynyaso na ukiukwaji wa haki za binadamu vinayoshuudiwa nchini si tu vinahitaji ushiriki wa kila mtu bali maombi ya dhati ili kulinuru taifa na hali hiyo.

Akizungumza mapema leo na waandishi wa habari mkoani Mwanza kwa niaba ya baraza la maaskofu Tanzania askofu msaidizi wa jimbo katoriki la Bukoba  Methodius Kilaini amesema kanisa katoriki linafadhaishwa na matukio hayo ya kiharifu yanayopoteza uhai wa watu wasio na hatia.

Amesema  “Ni vitendo vyenye kustahili kukemewa na kila mpenda amani  lakini anasema hiyo haitoshi tu bado yanahitajika maombi ya dhati kila mtu kwa imani yake ili kuliongoza taifa katika misingi sahii”.

Anasema kanisa katoriki limeifanya amani na mwelekeo wa taifa la Tanzania kuwa miongoni mwa masuala yatakayopewa kipaumbele katika ibaada rasmi itakayofanyika wakati wa kongamano la ekaristi takatifu june 11 mwaka huu jijini Mwanza.

Ni kongamano litakalo dumu kwa  takribani muda wa siku nne likihusisha kuyajadili na kuyaombea masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa.

Katika taratibu za kikanisa, tukio la ekaristi ndilo tukio kubwa kuliko yote katika misingi ya kanisa katoriki, awamu hii likifanyika jijini Mwanza, ikiwa ni mara ya tatu kufanyika nchini Tanzania, ambapo  pamoja na mambo mengine waumini,maaskofu,mapadri na watawa watakusanyika kuomba matumaini mapya kwa  jamii na familia nyingi zilizokata tama.

Akizungumzia suala la utendaji wa Rais Magufuli askofu Kilaini amesema ni mapema sana kumnyooshea mkono kiongozi huyo kwani miezi sita haitoshi kupima uwezo wa mtu aliyepewa kuliongoza taifa kwa miaka mitano.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU