Jamii Manyoni yaaswa kuwathamini watoto yatima
MRATIBU wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Manyoni
Orphans Sponsorship Association (MOSA) kilichopo wilayani Manyoni mkoani
Singida Bi.Mahewa Mowo ametoa wito kwa jamii kuwajali na kujitolea kuwapenda
watoto yatima.
Mratibu huyo ametoa kauli hiyo hivi karibuni kituoni
hapo alipotembelewa na gazeti hili na kufanya mahojiano maalumu yenye lengo la
kuikumbusha jamii juu ya watoto yatima.
Hata hivyo mratibu huyo amesema kuwa jamii inajisahau
na kuutupa utu wa mtoto yatima huku baadhi yao wakitendewa vitendo viovu na
walezi wao ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata elimu.
"Jamii imejisahau sana na kuutupa utu wa mtoto
yatima ,tafadhali tusiwatenge ili wasijione wapweke, tupo kwa ajili yao,"
amesema.
Pamoja na hayo Bi.Mowo amesema mtoto yatima ni mtoto
wa jamii na hivyo jamii inapaswa kumwangalia kwa ukaribu ili kutimiza mapenzi
ya Mwenyezi Mungu ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako.
“Watoto yatima ni wa jamii nzima, hatupaswi kuwabagua
wala kuwanyanyasa kwani wamezaliwa na ndugu zetu na hivyo ni wajibu wetu
kuwapenda na kuwajali na kuongeza ukaribu wa kuwa nao kwa kipindi chote
kigumu wanachopitia cha kuishi bila wazazi wao,” amesema.
Mbali na hayo amesisitiza kuwa serikali pia inapaswa
kushirikiana kwa ukaribu na jamii ili kuvumbua waovu wanaowanyanyasa yatima na
kwamba imefika wakati jamii nzima kuacha ukimya wa kuwafumbia macho watu
wanaowatendea vitendo vibaya watoto hao.
Ameyataja baadhi ya maovu wanayofanyiwa watoto yatima
kuwa ni pamoja na kubakwa, kulawitiwa na wakati mwingne kubaguliwa kielimu na
kukosa huduma za afya pamoja na kukumbwa na tatizo la ndoa za utotoni.
Peter Julius.ni mtoto wa m.o.s.a. manyoni.
ReplyDelete